Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Bwana Lusekelo Mwaseba (pichani) kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA).
Taarifa
iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, leo, Jumatano, Oktoba Mosi, 2014, na Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, imesema kuwa uteuzi huo unaanza leo.
Kabla
ya uteuzi wake, Bwana Mwaseba alikuwa Kamishna wa Uchunguzi katika Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA).
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2014.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...