Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Morrice Oyuke (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa Pato la Taifa kwa bei ya Soko leo jijini Dar es salaam. Wengine ni Bw. Fred Matola, Mtakwimu Mkuu Takwimu za Uchumi (kushoto), Bi. Adella Ndesangia (wa pili kutoka kulia) ambaye ni Mtwakimu Mkuu wa Ofisi hiyo na Bi. Jovitha Rugemalila.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO

Sekta za Kilimo,Viwanda, Biashara za jumla na rejareja zimetajwa kuongoza katika kuchangia kukua kwa pato la Taifa kwa asilimia 6.9 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2014.

Akitoa taarifa ya kukua kwa pato la Taifa leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Morrice Oyuke amesema kuwa kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2014 sekta hizo zimetoa mchango mkubwa wa kukuza pato la Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...