Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akifafanua jambo kwa washiriki (hawapo pichani),wa semina ya Fursa iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa hoteli ya KBH,iliyoko nje kidogo ya
mji wa
Singida,ambapo watu mbalimbali wakiwemo wanavyuo walishiriki.
Mmoja wa washiriki wa Semina ya Fursa akiuliza swali kwa Meza kuu ya watoa mada kuhusiana na mradi wa ufugaji wa kuku.
Mwakilishi kutoka Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF),Bwa.Ally Mkulemba akizungumza faida mbalimbali za kujiunga na shirika hilo la NSSF,alisema kuwa vijana wanapaswa kuamka kwa sasa na kuanza kuzichangamkia fursa zitokanazo na shirika hilo,ikiwemo mikopo,bima ya Aya na mengine kwa maendeleo na ujenzi wa maisha bora.
Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata
Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakimsikiliza Msanii mahiri wa Mashairi pichani,Mrisho Mpoto,alipokuwa akizungumza
ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya KBH,ilioko nje kidogo ya mji wa
Singida.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la
Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua
mjini Singida.
Msanii
wa Muziki wa Kizazi kipya kutoka kundi la Hip hop lijulikanalo kwa jina
la WEUSI,Niki wa Pili akizungumza mbele ya mamia ya washiriki wa semina
ya fursa iliyofanyika katika hoteli ya KBH nje kidogo ya mjini wa
Singida,Niki amewataka vijana mbalimbali kuhakikisha ndoto zao haziishii
njiani na badala yake wazifanyiekazi ili kujiletea maendeleo katika
maisha yao ya kila siku,pia amewataka kuitumia vyema fursa wanayoipata
katika njia mbalimbali.v
Mmoja wa washiriki wa semina ya Fursa,akiulaza swali na pia kuielezea fursa aliyonayo katika harakati za kutafuta maendeleo.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Automobile Garage,Joseph Msuya akifafanua jambo
kuhusiana na namna alivyoaianzisha kampuni yake na kufikia hapo
alipo,akitumia teknolojia za kisasa kabisa katika suala zima la ufundi
wa magari,utengenezaji Viyoyozi vya magari na mambo mengine mbalimbali.
Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata
Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakiwa ndani ya ukumbi wa hoteli ya KBH,iliyoko nje kidogo ya
mji wa
Singida wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumzwa.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la
Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua
mjini Singida.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...