Mrisho
Mpoto akimkabidhi kifaa cha kupimia magari mmoja wa wakazi wa Dodoma
Beatrice Chilewa (kulia), muda mfupi baada ya kujishindia moja ya swali
lililoulizwa na msemaji wa GS1, Pius Mikongoti, ambalo lilikuwa
likimtaka ataje nchi tatu za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazotoa
Barcode na namba za utambulisho wa nchi hizo, wa kwanza kutoka kushoto
ni Mkurugenzi wa kampuni ya Josekazi Auto Garage ambaye ndiye mmiliki
wa kifaa hicho cha kupimia magari.
MKURUGENZI wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba,(wanne kushoto) akiongea na baaddhi ya wakazi wa Dodoma mjini (hawapo pichani) waliohudhuria Semina ya Kamata Fursa ndani ya Ukumbi wa Royal Village mapema jana,ambapo aliwaeleza wakazi hao namna ya kuwapatia mbinu mbalimbali za kujikwamua kupitia rasilimali zilizopo ndani ya mkoa huo wa Dodoma.
Msemaji kutoka GS1, Pius Mikongoti akiwalezea wakzi wa Dodoma namna ya kunufaika kupitia huduma zitolewazo na GS1, hasa katika mfumo wa kutumia Barcode. 
Msanii wa kughani Mashairi Mrisho Mpoto akiwapa historia yake ya mafanikio na namna alivyoweza kutumia fursa hadi kufikia hapo alipo kwa sasa.
Sehemu
ya watu waliojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa
ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royal Village,mjini Dodoma hapo jana.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...