



……………………………………………………………..
Serikali imepiga marufuku ukataji
wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake anatakiwa
kuomba kibali kwajili ya kukata mti huo.
Akizungumza wilayani Siha juzi
,Waziri wa Maliasili na Utalii , Lazaro Nyalandu amesema kwamba Tanzania
inawez a kuwa jangwa baada ya miaka 15 kutokana na uvunaji mbaya wa
bidhaa za miti unaofanyika nchini .
“Tukiendelea kukata miti kma hivi
tutakuwa tunatengeneza janga la kitaifa kwa hiyo kwa sasa naomba niseme
rasmi kuwa hakuna mtu anaruhusiwa kukata miti au mti hata kama ameupanda
nyumbani kwake, ni lazima aombe kibali kwa maafisa wa misitu.
Tunatakiwa kushiriki kwa pamoja katika kutunza mazingira yetu” alisema.
Nyalandu alisema kasi ya ukataji
miti nchini imekuwa kuubwa kwa sasa kutokana na kuongezeka kw aidadi ya
watu na kuwa kwa mwaka mmoja pekee hekta 350,000 hukatwa huku kikiwa
hakuna jitihada za kurejesha iliyoondolewa.
“Kwa kaddri siku zinavyozidi
kwenda na watu kuongezeka baada ya miaka kumi misitu itakuwa inavunwa kw
azaidi ya hekta 850,000 nchini kwa mwaka, hii ni hatari kubwa, lazima
tufanye jitihada zaidi kukomesha tatizo hili”.
Aliwaagiza wakuu wa wilaya za
Arusha na kilimanjaro kuunda timu ili kuandaa hadidu za rejea kwa ajili
ya kupatia kikosi kazi ambacho kitaandaas andiko kw ajili ya kuanzisha
mfuko huo.
Mtendaji Mkuu wa wakala wa misditu
(TFS) Juma Mgoo alisema kwamba misitu ilianza kutunzwa mtokea enzi za
wakoloni lakini tatizio kubwa linalotokea kw asasa ni watu wengi
kuivamia kutokana na mahitaji ya nishati na uchomaji wa misitu.
Alisema kwamba kwa msitu wa asili
kawaida huwa na mita 30 za ujazo wakati kwa upande wa misitu ya
kuoandwea huwa wna ujazo wa zaidi ya mira za ujazo 400 hadi 600 kitu
ambacho alishauri umuhimu w akupanda miti zaidi ili iweze kukabiliana
na ongezeko la mahitaji na kuokoa misitu iliyopo.
Waziri Nyalandu alitoa maagizo ya
kuruhusu nguzio za umeme kupita katika msitu wa wilayani Siha ili
kufanywa wananchi waweze kupata nishati ya umeme ili kuokoa matumizi ya
kuni kama nishati na kulinda misitu.
“Umemem ni nishati mbadala badala
ya kuni na mkaa kwa hiyo napenda kuwaeleza kwamba ni bora miti michache
ikatwe ili pupisha nguzi za umeme ili wananchi wakipata nishati hiyo
waache kutumia kuni na kuharibu misitu na kutumia umeme kama nishati
mbadala” alisema.
UKWELI NI KWAMBA HAPO WAZIRI NYALANDU AMEC HEMSHA HUO NI UTAWALA WA KIDIKTETA, HUWEZI KUMZUWIA MTU KUKATA MTI WAKE WAKATI YEYE ALIUPANDA KWA MALENGO YAKE, UKWELI NI KWAMBA WENGI WETU ATATUFUNGA NA SHERIA IPO TUTABURUZANA MAHAKAMANI. BADALA YAKE ANGEWEKA MAZINGIRA YA KUHIMIZA WANANCHI WAKE KUPANDA MITI NA SIO KUKATA MISITU YA ASILI, MITI NIMEPANDA KWA MALENGO YANGU UKIFIKA MDA NITAKATA NIONE ATAKAE NIZUWIA, INATAKIWA IFIKE WAKATI VIONGOZI WENYE AMRI ZA KIDIKTETA WANG'ATUKE.
ReplyDeleteBIG UP NYALANDU! UMEFANYA BUSARA SANA NA UMEONESHA UZALENDO KWA NCHI YAKO. SHERIA HII ITASAIDIA SANA KUWEKA MAZINGIRA YETU KATIKA HALI YA USAFI. AIDHA SHERIA HII SIO NGENI KWANI IMESAIDIA NCHI NYINGI SANA KUBORESHA MAZINGIRA MFANO HUKU CHINA. MTU HARUHUSIWI KUKATA MTI NA WANACHOFANYA KUNA IDARA MAALUMU YA MISITU NDIO WANAHUSIKA UKATAJI MITI. JAMAA WANAHESHIMU SANA MITI. NAIKITOKEA KUWA MTI INABIDI UONDOLEWE BASI MTI HUO HUONDOLEWA NA KUOTESHWA SEHEMU NYINGINE. INABIDI TUFIKE MAHALA TUWAIGE RWANDA KWA UTUNZAJI MAZINGIRA NA KUWEKA NCHI SAFI. BIG UP NYALANDU IKIWEZEKANA WEKA SHERIA YA USAFI WA LAZIMA KILA MWISHO WA JUMA.
ReplyDeleteAmri hizi zinazotolewa kwa kukurupuka zinasababisha viongozi ngazi za chini kuzitumia kunyayasa wananchi. Kiongozi inabidi upime madhara ya amri kabla ya kuitoa!!
ReplyDeleteKweli kabisa mdau hapi juu. Waziri amechemka haswaa. Mti niupande mwenyewe kwa starehe zangu, niugharamie na kuuangaikia muda siutaki natakiwa niombe jibali...??? Huo ni uonevu. Km serekali mnatakiwa muwe na mikakati ya kuendeleza na kuboresha misitu na si kuwapa amri wananchi kwenye makazi yao. Tanzania tuna maeneo mengi yanayoweza kupandwa miti ila hakuna mikakati wala malengo mnaishia kunyanyasa na kuwabana raia.
ReplyDelete
ReplyDeletehahahahaaaaaa Nyalandu umenichekeshaaaa!!!
hahaaahaaaaaa! u r not serious!! r u?hahaaaaaa!