JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA
HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N
G O M E” Makao Makuu ya
Jeshi,
Simu ya Mdomo :
DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex
: 41051
DAR ES SALAAM, 20 Octoba, 2014
Tele Fax
: 2153426
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo
vya Habari
Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa ni
kosa kisheria kumiliki au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika.
Aidha,
kumeonekana matukio kadhaa ya baadhi ya vikundi, ama mtu mmoja mmoja
kumiliki au kuvaa sare za JWTZ.
Inakumbushwa kuwa kwa yeyote atakayeonekana amevaa ama kumiliki sare
hizo sheria itachukua mkondo wake.
Imetolewa
na Kurugenzi ya
Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P
9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963
NI VIZURI SANA KUWAKUMBUSHA RAIA MAANA IMEKATAZWA MUDA NA SHERIA IMEPITISHWA . ILA UMEKOSEA BADALA YA JESHI UMEANDIKA JENZI BUT IMEELEWEKA
ReplyDeletejamani wakuu wa jwtz mnapoandika taarifa kwa vyombo vya habari jaribuni kuweka mambao wazi,lazima watajwe hadharani wenye tabia za kumiliki na kuvaa sale za jeshi kama vile vikundi vya Muziki,wanamuziki ndio wenye tabia kama hizi,hatujui labda majambazi nao ujifanya kuwa wanajeshi,mnapokemea jambo lazima muweke wazi pasiwe na usiri wakati inajulikana wazi wanamuziki ndio walengwa katika taarifa hii
ReplyDeleteKazi kwakwe Diamond Platinumz na alichovaa fiesta.
ReplyDeleteSijui kama nakumbuka ya zamani, pale askari wangejichukulia sheria mkononi na kumiga na kumvua mtu yeyote ambaye ameva nguo zinazofanana na sare ya kivita(camoufalge, au combat)?
ReplyDeletetangaz hili limekuja sambabmba na picha ya ankal ikionyesha wanamziki wakiwa wamevaa surali zenye madoa kama ya jeshi.
Muono wangu hii sio sare ya Jeshi..sare ya jeshi itakuwa niz zile nguo zimetengenezwa kwa minajiri hiyo na watu wakaiba au askari wakaziuza mitaani.
Kusema nguo yeyote yenye madoo ni ya jeshi nadhani ni kukosea, kwani hatuweza kusema kuwa nguo ya rangi ya Kijani ( surali za jeshi) au nyekundu) nguo za sikuu za kijeshi) ni sare ya jeshi na hivyo tu atakuwa anavunja sheria.
ni muhimu tangazo kama hili litoe ufafanuzi zaidi ili wanachi wasio kuwa na hatia au kukusudia hatia kupigwa bure au kudhuluia bure nguo zao..
kama nitakuwa nakumbuka ya zamni basi itakuwa poa..
Ankal na wapiganaji wengine, fafanua au tafuta ufafanuzi kama mwandishi wa habari mpashaji/muhelimishaji wananch
kuna watu wana sare za mitumba toka USA na IRAQ. Msije kuwaonea.
ReplyDeleteje kupigwa au kuogelea kwenye maji machafu ndio sheria imechukua mkondo wake?
ReplyDeleteHauna cha sale za mtumba au MTAMBAAA.
ReplyDeleteWote hao wanaosea wavae nguo zngne.
JESH CHUUEN HATUA SYO MANENO TUUUUUUUUUUUU
AHSANTE WASEMAJI WA 2 WA MWISHO. NI KWELI KWAMBA SIO KILA NGUO YENYE MADOWA NI YA JESHI, NAUNGANA NA WENZANGU KUWA ( AVULIWE ALIEVAA SARE HALISI YA JWTZ) KAKA MICHUZI UNAKUMBUKA SWALI ULILOULIZWA USA NA AKINA JABIR, KUWA UNAANDIKIA CCM AU WATANZANIA WOOTE? NINGEOMBA UENDE JWTZ WAKUPE UFAFANUZI NI NGUO GANI ISIORUHUSIWA, UKWELI NI KWAMBA TZ INAONGOZWA NA WATAWALA SIO VIONGOZI KWANI MTU ANAWEZA KUIBUKA NALO ROHONI AKALIMWAGIA WALALAHOI WASIO JUWA HAKI ZAO NA HAWANA PAKUSEMEA. DON'T BE APSET COZ WE HAVE RIGHT TO EXPRESS OUR FEELING.
ReplyDeletekwahiyuo ni sare za jeshi la JWTZ ndio zimekatazwa kuvalia hadharani. kwa wasanii basi vaeni za USA au IRAQ.
ReplyDeleteSawa tumeelewa tusivae za JWTZ Zile za mabaka ya kijani.... Kwa hio tukivaa basi sare za jeshi la uarabuni rangi ya kahawia na nyeupe itakuwa no problem eti eee....
ReplyDeleteHivi kwa nini sare hizi iwe marufuku kuvaa? Mngeziacha tu na nyie mfanye kz ya kumwelimisha mwananchi tofauti ya mwanajeshi na asiye mwanajeshi sare sio kitambulisho cha mtu jamani
ReplyDeletesare ni kitambulisho tosha ndo maana askari wana sare, pia wanafunz je, ni fahar sana kuvaa nguo za kjeshi ilihali we siyo mwanajeshi? msione kila kitu mwaonewa, sheria ifuatwe.
Deletesare ni kitambulisho
DeleteNaungana na msemaji wa tatu na wanne, tangazo hili alipowazi ktk kuelezea nguo za jeshi ni za aina gani mitumbani nguo zenye kufanana na hizo wanazoziita za jeshi ni nyingi tu isije wakawadhuru watu kwa kuvaa nguo zenye kufanana na zao halikua ya kua zinatoka nje kama mtumba, ni vizuri watakae muhisi kwa kuvaa nguo zenye kufanana na sare zao wasikimbilie kujichukulia hatua kama ambavyo imezoeleka wachunguze imetengenezwa wapi....
ReplyDeletemadukani nguo zinazofanana na sare za jeshi ziko kibao! lakini sio sare za jeshi, mjadala huu umeanza tu pale Diamond platinamz alipovaa, amekamua kisawasawa ndo maana kelele nyingi, go Diamond, songa mbele!
ReplyDeletehuyo wanamsema platinum diamond mbona hawajamfanya chochote
ReplyDelete