Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inawataarifu Viongozi wote wa Umma nchini kwamba tarehe ya mwisho ya kurejesha Fomu za kutolea TAMKO LA RASILIMALI NA MADENI ya viongozi kwa Kamishna wa Maadili kwa mwaka huu ni tarehe 31/12/2014. Fomu hizo za kutolea tamko zimeanza kutolewa na zinapatikana katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma makao makuu Dar es Salaam na katika ofisi za Kanda za Mashariki Kibaha, Arusha, Dodoma, Tabora, Mwanza, Mbeya na Mtwara. Pia Fomu hizo zinapatikana katika Tovuti ya taasisi kupitia www.ethicssecretariat.go.tz na katika tovuti ya Serikali ya www.tanzania.go.tz

Viongozi wa Umma wanapaswa kuelewa kuwa ni Ukiukaji wa Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Kiongozi kushindwa kurejesha Fomu za Tamko lake katika muda uliowekwa na Kiongozi atakayeshindwa kurejesha kwa tarehe husika atachukuliwa hatua kama ambavyo kifungu cha 15 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995 kinavyoeleza. 

Viongozi wa umma wanapaswa kukumbuka kuwa sio wajibu wa kisheria kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi kuwa pelekea viongozi fomu za tamko bali ni wajibu wa kiongozi husika kuzitafuta fomu hizo kwa wakati  ili kutekeleza matakwa hayo ya kisheria.


IMETOLEWA NA
KAMISHNA WA MAADILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...