Wasaniiwa muziki wa asili wakitoa burudani katika tamasha la Jambo festival.
Mwenyekitiwa Tamasha la sanaa na utamaduni Arusha  maarufu kama JamboFerstival   Augustine Michael Namfua

Jiji la Arusha litatikiswa na tamasha la sanaa  na utamaduni la
kimataifa maarufu kama Jambo festival litakalojumuisha ngoma za asili,mavazi ya asili ,muziki wa asili,mavazi na vyakula  ,tamasha hilo litatikisa viunga vya jiji la Arusha ambalo ni kitovu cha utalii.

Takribani watu 3000 kutoka sehemu mbali mbali nchini na nje ya nchi
wanatarajia kuhudhuria tamasha hilo ambalo hutoa burudani isiyo kifani
na lenye kila aina ya ubunifu .

Wageni kutoka nchi za Afrika Mashariki Kenya,Rwanda,Burundi,Nchi za
Ulaya,Marekani na Asia wanatarajia kuhudhuria huku wenyeji wao wakiwa
ni wakazi wa Arusha.

Mwenyekiti wa Tamasha  la Jambo Festival , Augustine Michael Namfua
anaeleza kuwa tamasha hilo limekua likifanyika miaka 2 mfulululizo na
kwa sasa  linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa sanaa na utamaduni.
Augustine anaeleza kuwa kila mwaka wamekuwa wakifanya tamasha hilo
lengo ni kuonyesha kazi za sanaa hususani tamaduni.

Tamasha hili limekua likiwaunganisha kwa pamoja wapenzi wa sanaa na
utamaduni wa Watu wa Arusha,Tanzania  na Afrika  kwa ujumla hasa
ukizingatia kuwa Arusha ni makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki
na ni mji wa utalii.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...