Familia ya Mzee Solomon Seth Gwassa wa Forest, Mbeya inasikitika kutangaza kifo cha babu yetu Mzee Seth Asombwile Gwassa(miaka 99) kilichotokea tarehe 27/10/2014 huko kijijini kwake Ilundo-Kiwira, Rungwe-Mbeya. Mipango ya mazishi inafanyika huko huko kijijini kwake, na mazishi yatafanyika tarehe 29/10/2014. Habari ziwafikie watoto wa marehemu popote walipo, wapwa wa marehemu popote walipo, wajukuu wa marehemu waliopo Mbeya, Dar es salaam, Vietnam na China, na vitukuu wote.
Mwanga wa Milele umwangazie ee Bwana.
Amen
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...