Mshambuliaji Machachari wa timu ya Mshikamano (kulia) akijaribu kutaka kumtoka beki wa timu ya Amani katika Mchezo uliowakutananisha viongozi wa Dini nchini ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha Amani na Mshikamano kwa Taifa la Tanzania uliocheza jana kwenye Uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.hadi mwisho wa Mchezo timu ya Amani ilishinda goli 1-0.Picha na Othman Michuzi.
Golikipa hodari kabisa wa timu ya Amani akidaka mpira kwa uhodari mkubwa katika Mchezo uliowakutananisha viongozi wa Dini nchini ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha Amani na Mshikamano kwa Taifa la Tanzania uliocheza jana kwenye Uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.hadi mwisho wa Mchezo timu ya Amani ilishinda goli 1-0.
Refarii wa kutumainiwa,Kamishna Suleiman Kova akiwa makini kabisa na mchezo huo.
Hayaaaa anakwenda Mshambuliaji wa Timu ya Mshikamano paleee..... anakwendaaaaa.... anaendelea kuichachafya ngome ya Amani.....
hasa sasa anakwenda paleeeee.....anaangalia ampe nani pasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...