Timu ya wavutaji kamba wanaume ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwavuta wapinzani
wao (hawapo pichani) Wizara ya Ujenzi wakati walipokuwa wanashindana katika Uwanja wa
Jamhuri Mjini Morogoro leo. Timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani iliibuka mshindi kwa pointi
moja.
Timu ya wavutaji kamba wanawake ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwavuta
wapinzani wao (hawapo pichani) Wizara ya Afya wakati walipokuwa wanashindana katika
Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro leo. Timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani iliibuka mshindi
kwa pointi zote mbili.
Muhamasishaji wa uvutaji kamba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Salma Hamza (katikati)
akilia kwa furaha baada timu zote mbili za wizara hiyo kuibuka kidedea katika mashindano ya
uvutaji kamba katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara pamoja na Taasisi zake
(Shimiwi) yanayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji wa Timu ya Netball ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dafroza Benard
(kulia) akiuangalia mpira aliourusha ukiingia katika nyavu ya timu ya Wizara ya Afya wakati
walipokuwa wakicheza na timu hiyo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo. Picha zote
na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...