Mchakato wa uuzaji na ununuaji wa
bidhaa umerahisishwa sana kwa kadri waendashaji wa makampuni ya biashara kwa
njia ya intaneti wanavyozidi kuwa wabunifu na wagunduzi zaidi.
Kaymu Tanzania, kampuni inayoongoza kwa
kuuza na kununua vitu kwa njia ya mtandao imejitanua zaidi baada ya kuzindua
app (programu ya simu) yake Septemba 2014.
Kaymu Tanzania imezindua huduma zake za
kwanza za programu ya simu nchini, hivyo kuwawezesha watumiaji wa Android kufanya
manunuzi ya bidhaa na kuweka oda moja kwa moja kupitia simu zao za viganjani,
na kuwawezesha pia wauzaji kusimamia maduka na oda zao kwa uharaka na uwepesi
zaidi.
Akizungumza na wanahabari kwenye makao
makuu ya kampuni hiyo hapo Mikocheni- Dar-es-salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Kaymu
Tanzania Erfaan Mojgani alisema, “Programu hii ina matumizi yote yanayotakikana,
kuwawezesha wanunuaji kutimiza muamala wowote ikiwemo: kutembelea maduka na
kuangalia aina tofauti za bidhaa mbali mbali, kuweka oda, na hata kuwasiliana moja
kwa moja na wauzaji katika mchakato huo"
Kwa kuongezea, application (programu)
hii – inayopatikana kwenye Google Play Store – haina makato yoyote ya pesa kwa
watumiaji wa "smartphone" wanaotumia mtandao wa Tigo. Mnunuaji au
muuzaji yoyote anaweza akadownload hii application, na akafungua akaunti yake
na kuitumia kwa kupitia intaneti.
“Faida za programu hii ni kubwa pia kwa
wauzaji, ikiwarahisisha uwekaji wa picha za bidhaa mpya na ikiwapa wepesi wa
kusimamia accounts zao, kuhariri orodha ya bidhaa, na kuona mauzo yao” Erfaan
aliongezea.
Kwa kutambua kuwa asilimia kubwa ya
ongezeko la watumiaji wa intaneti nchini Tanzania wanatumia intaneti kupitia
simu za mikononi, Kaymu imedhihirisha jinsi ilivyojikita kwenye suala la
ubunifu na kuwapa wateja wao uwezo wa kutumia hii app (programu) kwa urahisi
zaidi. Zaidi ya hayo, kuonyesha kuwa watumiaji wa iphone hawajasahaulika, Erfaan
aliongezea kuwa application hii kwa watumiaji hao tayari iko katika matengenezo.
Jamani Hawa jamaa ni magumashi tu . They dont deliver whatever you buy
ReplyDelete