Kamati ya Bunge ya Bajeti inatarajia kuanza vikao vyake kuanzia tarehe 13 Oktoba hadi 2 Novemba, 2014. Katika vikao hivyo Kamati inatarajia kushughulikia Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi (Tax Administration Bill, 2014) na Muswada wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (Value added Tax Bill, 2014). 
Katika kutekeleza azma hiyo, Kamati imepanga kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi (Tax Administration Bill, 2014) na Muswada wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (Value Added Tax Bill , 2014) siku ya Jumamosi hadi Jumanne ya tarehe 25 – 28 Oktoba, 2014 kuanzia saa 4:00 Asubuhi Ukumbi wa Mkwawa, Ofisi ya Bunge Dar es Salaam. Miswada hiyo itashughulikiwa kwa pamoja kutokana na maudhui yake kushabihiana. 
Kwa maelezo zaidi unaombwa kuwasiliana na Ndugu Michael Chikokoto simu Na.0785-570685 au Michael Kadebe kwa simu Na. 0713-705463.


15 Oktoba 2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mngeweka online link kwa blogs mbali mbali ili wasioweza huko wachangie .... mnaweza pata mawazo mazuri sana kutoka kwa wengine

    ni pendekezo tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...