IMG_2450
Daktari kijana Brian Mushi wa Projeckt Inspire akionyesha upendo kwa mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho kilichopo Msimbazi Centre mara baada ya kumpima Presha wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.

WAZEE wanaoshi katika makazi ya Msimbazi Centre Jijini Dar es salaam karibu na kanisa la Mtakatifu Maria wa Fatma, Msimbazi walipata faraja kubwa baada ya kutembelewa na makundi matatu ya jamii.

Makundi hayo ni pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini, Tushikamane Pamoja Foundation na madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy. Makundi hayo yalifika katika kituo hicho katika kuadhimisha siku ya wazee duniani.

Wakiwa na lengo kuu la kuwafariji, kukagua afya zao na kuheshimu uwepo wao, makundi hayo pia yaliwapa zawadi za vyandarua, sabuni za kufulia na kuogea, pampers, Thermos Flask, vikombe vya chai, sahani za kulia, vijiko, sukari, njugu mawe, Tshirts, viatu, nguo, vyombo vya kufanyia usafi .
Pia walipiga picha za pamoja za ukumbusho.

Siku ya Wazee Duniani imetengwa kwa ajili ya kuweaenzi na pia kuwakumbuka kwa mambo waliyofanya kuendeleza kizazi cha wanadamu.
IMG_2514
Dr. Brian Mushi wa Projeckt Inspire akimpima presha mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho.
IMG_2523
Dr. Brian Mushi wa Projeckt Inspire akichukua vipimo vya damu kwa ajili ya kupima sukari kwa mmoja wa wazee wanaolelewa kwenye kituo hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...