Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Rachael akitumbuiza jukwaani pamoja na mcheza shoo wake mbele ya mashabiki wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika ndani ya uwanja wa Jamhuri,mkoani Dodoma usiku wa kumkia leo.

Pichani ni kulia ni Msanii wa bongofleva AbdulKiba akiimba sambamba na kaka yake Alli Kiba ambaye amekuwa akifanya vyema katika anga ya muziki wa kizazi kipya kupitia nyimbo zake mbili alizoziachai hivi karibuni,ikiwemo MwanaDaisalama na Kimasomaso,
Mkali mwingine wa muziki wa hip hop nchini Tanzania,Fid Q akiwashushia mistari wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta 2014,ndani ya uwanja wa Jamhuri usku wa kumkia leo.

Msanii wa bongofleva kutoka kampuni ya No Fake Zone Lina Sanga akiimba wimbo wake wa Ole Temba ambao umepokelewa vyema na mashabiki wake,ndani ya tamasha la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Sehemu ya umati wa watu waliofika kushuhudia tamasha la Fiesta 2014 ndani ya uwanja wa Jamhuri usiku wa kuamkia leo mkoani Dodoma.
Shangwe za mashabiki zikiwa zimetawala uwanjani hapo.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...