Msanii
wa muziki wa kizazi kipya kutoka kampuni ya No Fake Zone,Lina Sanga
ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Oletemba,akiimba jukwaani
mbele ya umati wa watu wakati wa tamasha la Fiesta lililofanyika jana
katika uwanja wa Namfua,kulia ni mmoja wa wacheza shoo wake akiwajibika
jukwaani.
Kundi
mahiri la muziki wa kizazi kipya litambulikalo kwa jina la Makomando
wakilishambulia jukwaa la Fiesta hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua
mjini Singida.
Sehemu
ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la
Fiesta ndani ya Uwanja wa Namfua hapo jana mjini Singida.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya vipaji ya THT,Rachael
akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani),wakati wa tamasha la Fiesta
likendelea ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
Msanii
mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes anaetamba na wimbo wake
wa Togola akiwaimbisha mashabiki wake,kwenye tamasha la Fiesta ndani ya
uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
Msanii
Mwana-FA na Linah wakiimba kwa pamoja wimbo wao wa Yalaiti jukwaani,huku miluzi na makelele
ya mashabiki yakiwa yametawala kila kona ya uwanja wakati wa tamasha la
Fiesta likiendelea.
Wasanii
mahiri wa muziki wa Bongofleva,Ney wa Mitego na Stamina wakilishambulia
jukwaa kwa pamoja kupitia wimbo wao unajojulikana kwa jina la Huko
kweni Vipi,ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya
uwanja wa Namfua mjini Singida.PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...