Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam,wakioneshwa na Meneja miradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza moja ya progamu zinazopatikana katika Kompyuta zinazowawezesha kupata taarifa ya masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao wakati alipotembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam Theresia Ng’wigulu (kulia) Meneja miradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza(kushoto ) pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (katikati)wakimsikiliza mmoja wa wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa,Matha Galus akiwaelezea jinsi anavyoweza kupata taarifa za masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao, wakati walipotembelewa na maofisa wa Vodacom shuleni hapo kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
Baadhi ya Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Theresia Ng’wigulu watatu toka kulia pamoja na maofisa wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu wa kwanza kushoto na Renatus Rwehikiza(kulia)wakimsikiliza Mwalimu wa somo la kompyuta wa kidato cha pili Nicolas Wilson wa shule hiyo akiwafafanulia jambo kuhusiana na elimu ya mafunzo ya kompyuta wakati walipotembelewa na maofisa hao kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
Wanafunzi wa kidato cha pili wakiwa darasani katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam,wakiwa na nyuso za furaha walipotembelwa na Maofisa toka Vodacom Foundation kwaajili ya kujionea maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...