Je ! Huu ndio uwekezaji wenyewe ? Idara ya Uhamiaji mpo wapi ?

ah !  "MGENI WA MUNGU HUYU" mwache ajitafutie riziki ! 

Baadhi ya wawekezaji wa kigeni au pengine watumishi raia wa kigeni wamekuwa wakivunja sheria za nchi kwa kujiingiza au kufanya shughuli zisizo katika mikataba yao ya kazi,au nje ya vibali vyao vya kufanyakazi hapa nchini Tanzania,lakini uvunjwaji wa sheria za nchi unaofanywa na wageni hawa unasaidiwa na sisi wenyewe kwa kuzingatia zile mila zetu na misemo ya ah !  "MGENI WA MUNGU HUYU" mwache ajitafutie riziki.
 
Matokeo yake tumekuwa na wachoma mahindi  mtaani kutoka china,wabeba zege pia,Kumradhi pengine makahaba au changudoa kwenye madangulo ya siri.
 
tunaweza kuwa na wakaanga samaki, walinzi "Kolokoloni" kutoka Thailand na Bangladesh,inawekana kabisa tunao hapa nchini wapishi na tour guider kutoka nchi za ulaya !Kwa mtindo na utamaduni wetu huu wa ah! wache "WAGENI WA MUNGU " wajitafutie ridhiki   tutajikuta tunao akina mama ntilie wa kigeni.
 
Tunajiuliza wale wawekezaji wanajiusha na biashara za mitumba au maduka ya nguo kariakoo hivi vibali aliwapa nani? yaani muuza mtumba na duka la sukari atoke china,Yemen,Bangladesh ulaya ! hii kweli inaingia akilini kwa watanzania? Sasa wawekezaji hawa kigeni wanafanya shughuli hizi mcha wa jua kali tena kweupe.
 
Mkondo wa sheria ya nchi unavunjwa walinzi wa sheria wako wapi?
Wizara zinazohusika amlioni hili au ndio ah! TUWAACHE WAGENI WA MUNGU wajitafutie ridhiki ?  Watanzania ukarimu ni jadi yetu ! misemo hii haifanani kabisana ukiwikaji wa sheria za uhamiaji na ajira za nchi, kwani katu kwame uruma nahaki havikai pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Wee si unajua kuwa Serikali yenyewe iko likizo..ndio maana wakihojiwa husema hata wao hawajui kwa nini Tanzania bado ni nchi masikini..Strange!
    Tanzania ni shamba la bibi (lisilo na mwenyewe) yeyote anaweza kuja atokako akavuna anavyotaka. no one in gvmt seems to care at all!

    ReplyDelete
  2. wacha soko huria litawale.

    ReplyDelete
  3. inawezekana mapishi ya kichina ni bora ndo maana biashara yake inafana.

    tumezoea kulindiwa kazi na biashara zetu, tukawa si wabunifu na si washindani, sasa twaona hatari, twataka serikali itumie sheria za ubaguzi wa kiutaifa kulinda kazi za kuchoma hindi. hivi serikali ina muda huo?

    ReplyDelete
  4. acha ukabulu.

    ReplyDelete
  5. Waswahili tupo tayari kuomba pesa kwa ndugu, ukiambiwa changamkia fursa choma mahindi upate rizikimunaona umedharauliwa au kunyanyaswa na ndugu yako. Akichoma mahindi mchina kutafuta riziki ooh akamatwe ooh mwekezaji gani? Hivi kila mzungu au mgeni aliyomTanzania ni mwekezaji? Kama kao dada yetu wa Kitanzania na yupo kihalali tutasemaje?

    Hapo kuna kitu cha kujifunza, tufanye kazi, huo ndiyo ujasiriamali, kesha au kesho atakuwa analeta makonteina kutoka china kuuza nyumbani na kutoa bidhaa kutoka Tanzania kwenda nje. Tufunguke na tuchangamke, hata ukiwa na digriimunaweza kuchoma mahindi na kupata rizikimyako badala ya kujibana na kuishi na wazazi wako ambao wamekusomesha hadinchuo kikuu, ukiona fursa ya kuchoma mahindi imejaa jaribu mihogomna zingine yote ni pesa tu... fursa siko kupata kazi na kuvaa taimwakati mfukoni hakuna kitu:-)

    ReplyDelete
  6. Baadae wanaingia ktk ujambazi na wanawake ktk uchangudoa!!

    ReplyDelete
  7. Kawaida mbona africa kusini wabongo wanauza Apple chini kabisa na hawafukuzwi na wengine wananyoa nywele nje kabisa nywele zinapepeluka nz wala hawafukuzwi na ulaya pia vile vile wabongo wanauza vitu nje bila mpangilio na hawafukuzwi na American vile vile hata australia sema wewe ulio andika hapo haujatembea na hauna elimu ya mtaan ndio shida ya watanzania wanaosoma kwa kukalili wacheni watupe changamoto ya akiri na sisi tuwe wachangamfu wa kujituma

    ReplyDelete
  8. Huyu jamaa ni mbona ni Mtanzania? Au rangi ya ngozi yake ndio tatizo?

    ReplyDelete
  9. Kamshikia muuzaji ili apigwe picha au yeye mwenyewe ndiyo anauza haya mahindi?

    ReplyDelete
  10. makahaba wa nje nenda Hunters kinondoni ndani kule wanapodance utawakuta kibao, kule ndipo maficho yao...

    ReplyDelete
  11. Mbona sisi kwao haturuhusiwi kufanya hivi? wawajibishwe...Hawa watu wa Uhamiaji wanakula tuu rushwa ndio maana wanawaachia...Si kama hawawaoni

    ReplyDelete
  12. sasa kulikoni tena katika uwekezaji huu?mbona wawekezaji wageni wameingilia ajira za wenyeji,hivi kweli walinzi wa katiba wanaliona hili bila kulichukulia hatua? hapa kweli kazi hipo.

    ReplyDelete
  13. huyu mchina ndio kusema anafanya anachotaka bila kujali chochote,na kariakoo ndio wamejaa

    ReplyDelete
  14. Ndugu unachoongea ni Kweli lakini zingatia yafuatayo.

    (a) Tanzania kama nchi nyingine mgeni anaweza kuwa na sifa za uraia, akaomba uraia akawa raia wa Tanzania. Baada ya kuwa raia wa Tanzania huwezi kumpangia cha kufanya yeye na familia yake kama hawavunji sheria.

    (b) Dunia imekuwa kijiji watu wanaoa na kuolewa na wageni, watoto wao ni raia wa Tanzania, huwezi kuwapangia cha kufanya pia.

    (c) Muwekezaji aliyekidhi viwango ana ndugu na jamaa wanaoishi wote, akitaka kujitafutia bila kuvunja sheria huwezi kumpangia kazi ya kufanya.

    zipo sababu nyingi kuwaona wageni wapo wanafanya kazi ambazo wazawa wanaweza pia kuzifanya. Nenda nchi za wenzetu ona watanzania wanavyofanya kazi za kufagia, kulea wazee, kulea yatima, kubeba mabox, ukorokoroni nk. na wanapata fedha wanaijenga Tanzania. Ukifika china dada zetu changudoa wapo na unalijua hilo. Nyie wataznania mnataka mkafanye kazi za kishenzi kwa wenzenu halafu wenzenu wakija mnataoa macho, acheni ubinafsi fanyeni kazi. Fika Guangzhou-China, London-Uingereza, na nchi nyingi za ulaya, fika majimbo karibu yote ya Marekani uone wabongo mnachofanya kule ndio utatulia. Kwa ufupi katika ushirikiano wa kimataifa kuna mambo huwezi kuyakwepa. Kula uliwe kaka.

    ReplyDelete
  15. Hii haiwezekani. Hata yeye mwenyewe "mwekezaji" haamini hii.

    ReplyDelete
  16. We uliyeleta hii mada, kumbuka kuwa sio kila mweupe unaemuona ni mwekezaji, kuna weupe wakazi wa tz.Weupe wengine ni watz wengine ni wakazi kama unavyoona nchi nyingine duniani, watu wamechanganyika wanapiga kazi nchi inaendelea.Mtu akishapewa ukazi anakuwa na rights nyingi za kufanya kazi, biashara ili mradi afate sharia za nchi.Ukienda china na nchi nyinginezo utakuta wa tz wamepewa ukazi na wana maduka na kazi nyinginezo wanafanya pia.Mara nyingi mtu akishindwa anaona labda mgeni ndio sababu ya kushindwa kwake.Wewe tafuta mtaji kasha ufungue na wewe sehemu yako uchome mahindi, tutakuja kununua. Wageni mara nyingi hujishughulisha, mtz anataka easy things, ndio maana ni wanyang'anyi, majambazi na Malaya. So fanya kazi coz uhamiaji hawatafanya lolote kama walishatoa kibali.

    ReplyDelete
  17. Mbona picha hiyo juu jamaa anaechoma mahindi ni mtailand na yuko Kwao Thailand angalia namba ya gari, hii habari inanaanisha mwandishi ana ubaguzi wa kibinadamu.

    ReplyDelete
  18. Wewe uliyeleta mada hii ungetumia muda wako kufanya kazi itakayokuingizia kipato baada ya kulalamika ovyo. ETI WANACHUKUA KAZI ZETU? Kwani watanzania kazi zetu ni kuchoma mahindi??? Waache wachome mahindi ili mradi hawaweki sumu kwenye hayo mahindi na wana customer service nzuri hakuna shida tutanunua tu hayo mahindi yake. Watanzania tukubali ushindani, tumekuwa very protective ndiyo maana vitu vidogo vinatushinda tukisikia East Africa Federation tunaanza kutetemeka, tunapenda kutoa visababu vidogo vidogo visivyo na msingi. Kama wanaleta biashara ya ukahaba kuna shida gani? Hiyo ni huduma kama huduma nyingine kama wewe binafsi huhitaji wengine wanahitaji.....waache wafurahie huduma wanazozitaka, wawe na furaha na vitu wanavyohitaji. Msiifanye nchi yetu ikawa kama Afghanistan au Somalia.

    ReplyDelete
  19. Acheni shobo wabongo wavivu kutwa kushinda vijiweni mchina kapiga bonye anaziokota chen chele mnamzonga wachawi wote mnao mpiga chabo.zola ley

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...