.Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa(kulia)akikabidhiwa Usinga unaomtambulisha kama mzee wa jamii ya Kimaasai(Laigwanani) na Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati mkoani Arusha,Solomon Masangwa wakati wa harambee ya kuchangia ukarabati wa Miundombinu iliyochakaa ya Shule ya Sekondari ya Enaboishu,Shule hiyo imeanzishwa miaka 48 iliyopita na KKKT.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akitoa hotuba yake wakati wa harambee ya kuchangia ukarabati wa Miundombinu ya Shule ya Sekondari Enaboishu,kushoto ni Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Solomon Masangwa,Mkuu wa Shule hiyo,Lesion Ole Sekioni na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo ambaye ni mhitimu wa Shule hiyo,Elisante Ole Gabriel.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Solomon Maswangwa akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Profesa Elisante Ole Gabriel aliyebuni mpango wa kuwakutanisha wanafunzi waliosoma Shule hiyo kuchangia maendeleo ya elimu,yeye akiwa mmoja wao.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na Wafanyakazi wa Shule ya Enaboishu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...