Waziri Mkuu, Miengo Pinda akitazama ngoma ya Kihaya kabla ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba Oktoba 5, 2014 ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za siku ya walimu duniani zilizofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Oktoba 5, 2014. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Mbunge wa Luangwa, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabiana Massawe.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu , Fabian Massawe (kushoto kwake) na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kagera, Costansia Buhiya (kulia kwake) kuvuka uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kutua kwenye uwanja huo, Oktoba 4, 2014 ambako Oktoba 5,2014 alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za siku ya walimu duniani zilizofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na baadhi ya viongozi wa chama cha Walimu Tanzania kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kuhutubia katika sherehe za siku ya walimu duniani zilizofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Oktoba 5, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Mbunge wa Bukoba mjini, Hamisi Kagasheki kwenye uanja wa ndege wa Bukoba kabla ya kuondoka kuelekea Dodoma Oktoba 5, 2014. Mheshimiwa Pinda alikwenda Bukuba kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za siku ya Walimu Duniani zilizofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Kaitaba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...