Na Editha Karo wa Globu ya Jamii, Kigoma

SERIKALI ya Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Word Lung Foundation chini ya ufadhili wa Swedish Internatinol Agency (SIDA) wamezindua Mkoani hapa kampeni ya''THAMINI UHAI OKOA MAMA MJAMZITO NA MTOTO''

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya alisema kuwa lengo la kampeni hiyo kuongeza na huduma kwa akina mama wajawazito waweze kujifungulia katika vituo vya huduma ya afya.

''Hawa ndugu zetu wa WLF wamekuwa wakitusaidia sana katika masuala ya afya ya mama mjazito na mtoto hapa kigoma,Mambo ya kujifungulia nyumbani yameshapitwa na wakati,nina waomba akina mama wote wanapo pata ujauzito kuanza klinik mapema ili waweze  kuonana na wataalam mapema''alisema machibya 

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali  ya Mkoa wa Kigoma Dkt Leonard Subi alisema kuwa shirila la WLF limekuwa mstari wa mbele katika kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto katika Mkoa wa Kigoma.

Alisema wanawake wanaojifungulia katika vituo vya afya Mkoani Kigoma ni wachache hali hiyo ndiyo inayosababisha idadi ya vifo vya akina mama wajawazito kuwa kubwa,wengi hupenda kujifungulia manyumbani sababu ya fikra potofu.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Word Lung Foundation nchini  Nguke Mwakatundu alisema kuwa shirika kupitia kampeni hiyo limedhamiria kupunguza matatizo ya uzazi wakatiwa kujifungua kwa akina mama.

Alisema kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu inawalenga wanawake na wanaume wote MkoanI Kigoma itafanyika kwa njia ya radio,mabango,simu za mkononi,katuni na uhamasishaji.

''Nina amini kampeni hii itafanikiwa katika Mkoa wa Kigoma japo kuna changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa watumishi katika vituo vya afya,vitendea kazi pamoja na akina mama kuchelewa kufika katika vituo vya afya kwa wakati kujifungua''alisema Mkurugenzi Mkuu
Wahudumu wa Hospita ya Mkoa wa Kigoma maweni pamoja na wananchi wakitembea kwa maandamano kuelekea katika viwanja vya sekondari ya mwananchi Mkoani Kigoma kwaajili ya uzinduzi wa kampeni ya ''THAMINI UHAI OKOA MAISHA YA MAMA MJAZITO.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akizindua kampeni ya ''THAMINI UHAI OKOA MAISHA MAMA MJAMZITO''katika viwanja vya sekondari ya mwananchi wa nyuma yake ni Katibu Tawala wa Mkoa Mhandisi John Ndunguru.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma pamoja na viongozi wengine wa serikali ya Mkoa wa Kigoma wakipiga makofi baada ya uzinduzi kufanyika.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali msataafu Issa Machibya akimpongeza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Word Lung Foundation Nchini Dkt Nguke Mwakatundu baada ya uzinduzi wa kampeni na anayefuata ni Mganga Mkuu wa Hospita ya Mkoa wa Kigoma Dkt Leonard Subi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...