Bwana na Bibi Rick Tingling wakiwashukuru watu kwa kuja kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambayo hiyo jana siku ya Jumapili Novemba 2, 2014 ilikua ni kumbukumbu ya 6 tangia bwn. Rick Tingling alipoanzisha kumbukumbu za Mwalimu Nyerere mwaka 2009 hapa DMV. Yeye bwn. Tingling ni Mmarekani aliyemjua Mwalimu Nyerere kwa kusoma vitabu vyake na kuanza kumfuatilia na kutambua kwamba Mwalimu Julius Nyerere ni kiongozi asiyekua na mfano na ambaye huwezi kumlinganisha na kionozi yeyeyote hapa Dunia si zama hizo au wakati huu tulio nao sasa. Bwn. Rick Tingling amesema ataendelea kumenzi Mwalimu Julius Nyerere kila mwaka.
Dr. John Rutayuga ambaye ni CEO wa Ukimwi Orphans Assistance akielezea kazi ya kikundi hicho inayofanya nchini Tanzania na baadae kuelezea kuhusu Mwalimu Julius Nyerere.
Msanii wa mashairi Anna Mwalagho kutoka Kenya ambaye ni mkaazi wa DMV akitoa shairi la I have a dream lililoelezea utajiri wa Africa na kwamba ndoto yake siku moja ni Africa itakua moja na itaitwa United State of Africa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...