Katibu
Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza alisema kwa mwenendo huo bora
unaofanywa na Msama anatoa wito kuendeleza mwenendo huo ili kuisaidia
jamii.
Mungereza
alisema Msama anafanikisha hayo kwa sababu anaipenda jamii ambako
alitoa wito kwa wadau wa muziki wa Injili kujitokeza kwa wingi katika
tamasha hilo linalotarajia kuanza Desemba 25 hapa nchini ili kufikia
malengo stahili.
Katibu
huyo alisema mbali ya kuchangia jamii pia kupitia tamasha hilo
wananchi wa maeneo husika wanapata fursa nyingi katika maeneo yao kama
madereva bodaboda, texi na biashara nyingine.
“Wananchi
wa mikoa itakayofikiwa na tamasha hilo watambue kwamba ni lao, hivyo
wajitokeze kwa wingi kwani viingilio vitakavyopatikana vinasaidia wenye
uhitaji maalum kama yatima, wajane, walemavu na wengineo,” alisema
Mungereza.
Kuhusu
waimbaji, Mungereza alisema waichukulie sanaa kwamba ni kazi watumie
vipaji vyao hasa wakifikiria jamii kwani wanahitajika kutoa elimu ya
uraia kutoka kwao.
Katika
hatua nyingine, Kampuni ya Msama imepokea kibali cha kufanikisha
Tamasha la Krismasi mwaka huu ambako kampuni hiyo imejipanga kufanya
tamasha hilo katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Naye
mmoja wa Watendaji wa Kampuni ya Msama, Jimmy Rwehumbiza aliyepokea
kibali cha Tamasha la Kriamsi aliishukuru Basata kwa kufanikisha kibali
sambamba na kupokea ushauri na mapendekezo yanayotolewa mara kwa mara
yanayofanikisha matamasha hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...