BENKI ya CRDB imesaini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni
43 baina ya benki ya uwekezaji Ulaya (E.I.B)
kwa ajili ya kuwakopesha na kuwasaidia wafanyabiashara wanaofanya shughuli za
kukuza uchumi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki Mkurugenzi Mtendaji
wa CRDB, Dk. Charles Kimei alisema benki yake kwa kushirikiana na EIB imeamuwa
kusaidia jamii nchini hivyo mkataba huo ni mwanzo wa ushirikiano endelevu
utakaohamasisha upatikanaji wa ajira.
Alisema kufanyakazi na benki ya EIB kutasaidia kukuza
biashara katika maeneo muhimu kama uvuvi, usindikaji wa chakula, usafiri,
biashara pamoja na huduma zote za kiuchumi.
“Mimi kama kiongozi wa CRDB Tanzania ninamamlaka ya
kusaidia hizi sehemu za soko na kuongeza jitihada za kumaliza umaskini, pia
kuongeza shughuli za kiuchumi za wateja wetu ili kufikia lengo la kuongeza
mapato katika benki yetu,” alisema Kimei.
Kwa upande wake Naibu
Waziri wa Fedha Adam Malima alisema mkataba huo pia una lengo la kuisaidia
benki ya CRDB katika kuendesha shughuli zake mbalimbali.
Alisema ni jambo la faraja kuona benki kama EIB imekubali
kuiamini CRDB na kuipa mkopo wa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara.
“Tunachokiamini kuwa hii benki kutoka Ulaya siyo benki
ndogo ni kati ya benki kubwa zilizopo hapa duniani, sasa kama wamekuja hapa
kwetu na wakaonyesha nia njema ya kutusaidia endapo watabaini kuwa pesa zao azitatumika
kwa malengo yaliyokusudiwa watavunjika moyo,” alisema.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akiwasili ukumbini wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mkopo wa sh. Bilioni 43 kutoka Benki ya Uwekezaji Ulaya. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Martin Mmari na (katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis (kulia) akisaini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 43 na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya Benki hiyo kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara Wadogo na Wakati. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari na Wa pili kulia ni, Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Eric Beaume.
Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis (kulia) akibadilishana hati na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya benki hiyo kusaini mkopo wa billion 43 na benki ya CRDB kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara Wadogo na Wakati. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...