Meneja Mwanandamizi wa Masoko na Mawasiliano wa BOA Tanzania, Bw. Solomon Haule  akizungymza na waandishi wa habari (hawapi pichani) kuhusu kampeni ya benki ya ufunguzi wa akaunti mpya,ambayo inawawezesha wateja wake watano kujinyakulia zawadi mbali mbali.
Mteja wa Benki ya BOA aliejishindia zawadi ya simu aina ya Samsung Galaxy Grand Duos,Ibrahim Agwanda akiionyesha simu hiyo kwa wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Mwandamizi wa Fedha wa BOA, Bw. Cleopa Dickson.

Benki ya Afrika Nchini Tanzania (BOA Tanzania) imewatunukia wateja watano wenye bahati ya pekee zawadi  za aina mbalimbali kwenye kampeni yake inayoendelea kuhusu ufunguzi wa akaunti mpya na kuendelea kuweka akiba katika zabuni yake mpya ili kuhimiza tabia ya kujiwekea akiba ncini.

Meneja Mwanandamizi wa Masoko na Mawasiliano wa BOA Tanzania, Bw. Solomon Haule alipokuwa anaongea kwenye sherehe fupi ya kuwatunuku tuzo washindi mwishoni mwa juma kwenye makao makuu ya Benki jijini Dar es Salaam alisema kwamba wateja wapya na wa zamani wa Benki wote bado wana nafasi kubwa ya kushinda tuzo mbalimbali za papo kwa papo wakifungua akaunti mpya au wakiweka fedha kwenye akaunti zao.

“Tuna furaha kubwa kwamba baada ya kuchezesha bahati nasibu kwa mwezi Oktoba, 2014 washindi wenye bahati ya pekee wamejishindia vitu mbalimbali vifuatavyo: pikipiki, tuzo ya fedha taslimu, vocha 100,000 za kununulia zawadi mbalimbali, simu za aina ya Samsung Tablet na Samsung Galaxy Grand,” alisema.

Bw. Haule aliwataja washindi kuwa ni Tom Gathari (pikipiki), John Raphael (simu aina ya Samsung Tablet), Ibrahim Agwanda (simu aina ya Samsung Galaxy Grand Duos), Mary Mushi (tuzo ya fedha taslimu Tshs. 500, 000) na mshindi wa mwisho kuwa ni Innocent Msigwa ambaye alijishindia vocha za kununulia zawadi mbalimbali zenye thamani ya Tshs.100, 000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...