Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),Balozi Juma Mwapachu (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya Uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko maalum wa Chuo Kikuu cha Dodoma,unatarajia kuzinduliwa rasmi kesho Novemba 8,2014 kwenye hoteli ya Golden Tulip,Jijini Dar es Salaam,ambapo Mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa Awamu tatu na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Mh. Benjamin W. Mkapa.Dhumuni la Mfuko huo ni kuweza kukisaidia Chuo hicho katika kukabiliana na mahitaji ya kifedha na vifaa mbali mbali chuoni hapo.Wengine Pichani ni Kaimu Mkuu wa Chuo hicho,Prof. Idris Kikula (katikati) na Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM,Prof. Ludovick Kinabo.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Prof. Idris Kikula akisisitiza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) wakati wa kuzungumzia Uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko maalum wa Chuo Kikuu cha Dodoma,unatarajia kuzinduliwa rasmi kesho Novemba 8,2014 kwenye hoteli ya Golden Tulip,Jijini Dar es Salaam.Katiki ni  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),Balozi Juma Mwapachu na kulia ni Katibu wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),Bi. Christina Silvester.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...