Taarifa
zilizotufikia hivi punde ndani ya chumba cha habari cha Globu ya
Jamii,kinaleleza kuwa kaimu Mkurugenzi wa TPDC,Bwa.James Andilile na
Mwenyekiti wake
wa bodi Bwa.Michael Mwanda wamepelekwa rumande kwa kosa la
kutowasilisha
mikataba 26 kwa kamati ya bunge la hesabu za mashirika ya umma
PAC,kamati imeagiza wapelekwe huko na hatua zichukuliwe dhidi yao.
Kikosi kazi cha Globu ya Jamii kipo kazini kuifuatilia taarifa hii,hivyo tuendelea kupitia pitia hapa jamvini kupata Updates.
Hivi kamati ya Bunge inaweza kumuamuru mtumishi wa umma awekwe rumande kwa kushindwa kufanya jambo fulani na hiyo amri ikatekezwa? Na ni sheria ipi inairuhusi hiyo kamati kufanya hivyo. Naomba ufafanuzi wadau mimi hapo sielewi!
ReplyDeletekama sijakosea hakuna sheria inayozuia hiyo mikataba isiende bungeni; sasa mpka kuwekwa rumande tatizo lipo wapi kwa mtumishi wa wananchi?ni jambo la ajabu! MALI ZOTE ZILIZOKO KWENYE ARDHI HII NI ZETU SISI TUNAOISHI KATIKA ARDHI HII.
ReplyDeleteDu! Tuone itaishia wap? Kama wezi wa EPA walisaamehewa kwa wizi wao, hawa itaishia juu kwa juu.
ReplyDeleteSasa wanaficha ,nini? Kama taratibu zote zimefuatwa? Hiyo mikataba Ni kwa faida ya nani? Kama Ni kwa faida ya watanzania, basi wawakilishi WA wananchi wapewe nafasi ya kuiona.
ReplyDeleteMnaogombea kupewa Uongozi mmeona makali yake?
ReplyDeleteZama hizi ni bora nichukue Jembe nikalime kuliko kukubali kubeba madaraka ni sawa na kujitwisha mgongoni gunia la misumari!