Na Mwandishi Wetu, Kibaha
BENDI ya Muziki wa Taarabu ya Coast Modern Taarab ya Jijini Dar es Salaam inatarajia kutoa burudani Novemba 27 mwaka huu kwenye mji wa Msata wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha mkurugenzi wa ukumbi itakapofanyika onyesho hilo, Msukuma Pub Msukuma Mwinzarubi alisema kuwa maandalizi yamekamilika.
Mwinzarubi alisema kuwa burudani hiyo itaongozwa na gwiji wa taarabu Jokha Kassim ambaye anatamba na kibao chake cha Domo la Udaku.
“Burudani itakuwa ya uhakika kama mnavyoijua Coast Medern Taarab wanavyopagawisha mashabiki wa muziki huu ambao unapendwa kwa sasa,” alisema Mwinzarubi.
Alisema kuwa wapenzi wa muziki huo wa wilaya ya Bagamoyo na maeneo mengine wategemee burudani nzuri na ya kuvutia.
“Pia kutakuwa na burudani mbalimbali za muziki za wasanii wa Msata wakiwemo Wasafi Group na wasanii wengine ili kusindikiza burudani ambayo itatolewa siku hiyo,” alisema Mwinzarubi.
Aidha alisema kuwa lengo la burudani hiyo ni kuzindua vyombo vya muziki ambavyo viliharibika kutokana na ajali ya gari ambalo lilibeba vyombo hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...