Rais
wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok Dhar akipongezana na
Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa tatu kushoto) baada
ya kuzindua kadi maalum za Safari za kampuni hiyo zitakazomwezesha
dereva kupata huduma ya mafuta kutoka vituo vyote vya Gapco nchini kwa
unafuu. Wengine (kustoka kushoto) ni Rais wa kampuni ya RIL ya Mumbai,
Ashok Dhar, Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum Bisarara, Ofisa Mtendaji
Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na Mkurugenzi
wa kituo cha Gapco, Barabara ya Nyerere, Muntazir Bharwani.
Rais wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok Dhar akikabidhi
kadi maalum za Safari kwa Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum Bisarara na
Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki baada ya kuzindua kadi
hizo zitakazomwezesha dereva kupata huduma ya mafuta kwa unafuu katika
hafla iliyofanyika Kituo cha Mafuta Gapco cha Kamata, Dar es Salaam
jana. Wengine (kutoka kushoto) ni Rais wa kampuni ya RIL ya Mumbai,
Ashok Dhar, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk.
Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
Rais
wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok akionesha kadi maalum
za Safari za Gapco baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika
kituo cha mafuta cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana. Kadi hizo
zitamwezesha dereva kuweza kupata huduma ya mafuta kwa unafuu kutoka
vityo vyote vya Gapco Tanzania. Kutoka kushoto ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu
wa Gapco Tanzania, Vijay Nair, Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum
Bisarara, Diwani wa Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa tatu kushoto),
Meneja Miradi wa Gapco, Mohit Shirma, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la
makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...