Today is your future kwa taarifa yako.. Ulipokuwa mdogo ulisema nikiwa mkubwa nitakuwa na gari na nyumba nzuri wazazi wangu wataishi hivi na vile. Je unayo? Je imetokea? Maybe yes. But maybe no.
Kama haijatokea je bado hujawa mkubwa? Basi kama ni mkubwa ujue kuna kitu hujafanya.
Utasema tena nikifika miaka 40 nataka niwe na hiki na kile watoto wangu wasome international skul nk. Subiri uone miaka inavyoenda. Usishangae kufika 40 bado umeajiriwa kwa mtu na anakugombeza kwa nini mwanao anaumwa kila siku unachelewa kazini. Kazi nyingi. No bright future. No enjoyable present. Just existing and not living!
Hapo ndo unawaza kufuga ng'ombe wa maziwa Kibamba kwenye kiwanja chako cha miguu 12 kwa 15! Wenzako wa umri wako hapo unasikia wameanzisha bizness in Australia. Wamenunua kiwanja Mbezi Beach kwa 300M! Wanamiliki Apartment Johannesburg. Wakienda UK wanaenda kula The Ritz (Google that). Wanasomesha watoto zao the finest schools available wewe wa kwako wakati huo wamekosa nafasi Makongo wameenda Kibamba Secondary School wanapanda daladala sita kwenda na kurudi full kutukanwa na makonda.
Wenzako in their 40s wanasaidia wasio na uwezo katika jamii wewe ndo kwanza ukipokea simu kutoka kijijini una-mute! Wenzako in their 40s wakisikia kuna ujenzi wa nyumba ya ibada wanachangia 5M kimyakimya.. Wewe ukitoa laki moja basi mpaka mtaa wa saba watakujua! Halafu unashangaa wanazidi kuinuliwa. Mwenye nacho ataongezewa au hujui? Na asiye nacho..... (Malizia)
Wenzako in their 40s wana exposure ya uhakika. Walishafika kuanzia Sauzi, Botswana, Mozambique, Kenya, Ethiopia, Ghana, Naija, mpaka Egypt, The UK, Australia, Hawaii, Mexico, Croatia, The Netherlands, Switzerland, US, Panama mpaka Puerto Rico, Brazil na jirani zake, Hong Kong, Australia, Japan, China, (Incredible) India, Thailand, Singapore, New Zealand, Comorros, you name it..!! Wewe hata Kampala hujawahi fika. Kila siku Tegeta Posta ndo ruti yako miaka 15 mfululizo eti unatafutia watoto maisha! Unaishi au unaisha?
Acha mawazo mgando. Hiyo ajira ifanye serious sana tu lakini kwa muda tu. Jiandae kusimama mwenyewe. Kwani hujiamini? Na Mungu naye humwamini? Changamoto ni sehemu tu ya kufika kileleni. Don't be afraid. Don't dwell in that comfort zone!! Unasubiri kiinua mgongo? Utaenda kukiinvest wapi na kwa nguvu ipi. Na utaenjoy retirement kweli kama at 60 yrs ndo unafungua duka la vifaa vya ujenzi eti vinalipa. Kwa nini hukufungua ukiwa 30 ili uone vinalipa au la. At 60? With due respect.
Suffer the pain of discipline now. Or else you will suffer the pain of REGRET. Halafu ukianza kuregret ndo pressure zinakuja, stress, nk mwisho unawacha hata hao watoto in a far worse situation than your own lifetime.
Life Begins at 40 my friend.. How Old Are You?
Inbox me tushauriane fursa inayoweza kukupa hayo unayoona leo kama ndoto. Kamata fursa #twenzetu!
Good article, but we all can`t make it! we are just like a tree, some are roots, some are trunks, some are branches, some are fruits, some are seeds, and they all depend upon each other in order to survive.
ReplyDeleteKwa mtaji huu, hata kama una zaidi ya miaka arobaini, na bado hujatoka! wala usikonde yote ni maisha, mshukuru Mungu kwa yote aliyokupa na umuombee akuzidishie, ila endeleza libeneke la kazi na kujituma, no sweat one day yes! utatoka tu, hata kama si wewe lakini ni mjukuu wako, hiyo ni damu yako.
Stay blessed,
Jah is great.
Dr Gangwe Bitozi-
Kwa kiswahili zipo methali zake.
ReplyDelete1. Utavuna ulichopanda (ukiona huvuni basi hukupanda, au hukumwagilia, au hukupalilia, au hukulinda wanyama na wezi wasivune kabla yako. Kuvuna kunahita ufanye kila kitu mstahiki).
2. Majuto ni mjukuu (ningejua nikapanada wakati ule ili nivune sasa).
Tatizo ni kwamba kupanda kunaanza ukiwa na umri wa miaka 3 wakati hujui utatakiwa uvune baadaye, unadhani baba atakuwepo siku zote.
Dr Gangwe Bitozi, umesema neno hapa. Najitahidi si kwa ajili yangu tu. Kama si mimi, basi watoto wangu, kama si wao basi wajukuu wangu.
ReplyDeleteNimetoke familia ya wakulima. Si farmers ila peasants. Unanielewa. Familia ambayo mtu akizaliwa, atakuwa hadi kufa akiwa na miaka 60-80 bila ya kukakanyaga kimji kidogo kilichoko km 50-100 toka kijijini. Mimi nimejitahidi, nimetoka huko kijijini na nina kazi mjini. Kusema kweli pamoja na kwamba sijatoka kwa maana yako, watoto wangu wanaanzia sehemu tofauti kabisa. Si kule nilikoanzia mimi.
Sasa hivi Watanzania wanataka watoke wote kwa njia yoyote. Jamii imebadilika kuwa ya wezi. Majambazi ya bodaboda yanataka yatoke kabla ya 40. Wezi wa mtandao wanataka watoke kabla ya 40. Wafanyakazi wa benki wanataka watoke kabla ya 40 - wanapanga ujambazi katika benki zao. Housegirl anataka atoke kabla ya 40 - anamwibia mwajiri. Tumekuwa jamii ya wezi kwa sababu ya kuamini kuwa kila mmoja ni lazima atoke. Hata USA kuna 1%er na 99%er. Kutoka wote before 40 ni nadharia tu. Mtu akinunua kiwanja cha mil 300 na wewe ukataka wakati huna uwezo, utakuwa jambazi mwishoe.
Mawazo yote ni ya busara, hasa hii ya 3 nimeipenda sana. Lakini lazima tujue na kujihesabu kwa wale wenzangu wanaomuamili muumba mbingu na nchi na akawaumba wao. tujue kwamba hatukuletwa duniani kuishi maisha ya kutoka tu bali ni majaribio na matayarisho ili kuyafikia maisha ya milele. Utaratibu wa dini ninayoifuata mm inasema hivi:- UKIFIKA UMRI WA MIAKA 40 UNATAKIWA UJIFANYIE TATHMINI YA MEMA NA MAOVU YAKO KWANI KILA MTU ANAIJUA NAFSI YAKE VIZURI, SO KAMA MAOVU WAMEYAZIDI MEMA BASI UJITAHIDI UMRI ULIOBAKIA KUFANYA MEMA OTHERWISE UJIHESABIE NAFASI KWENYE JAHANAMU.
ReplyDeleteUnayemuona katoka kabla ya 40 basi ujue Baba yake alikuwa fisadi na Kama sio fisadi basi yeye ni fisadi! Kwa mshahara upi? Wote tunaijua mishahara ya Serikali au Makampuni Binafsi bila ya dili chafu (ingawa wengi wao wanaziita safi moyoni) hakuna maendeleo ya kweli!
ReplyDeleteKama tunabisha kwa yote niliyosema basi tuwaombe Mataifa ya nje yaje kuchunguza kila raia wa Tanzania anayejiita ametoka tuone chanzo cha pesa zake kilianzia wapi? Kama hatutajua ukweli wote!
Wengi wao wanaonga ili wapate nafasi nzuri makazini na mishahara minono sasa hapo ukitoka basi sio kazi yako bali ni ule ufisadi wako wa mwazo uliotoa rushwa ndio uliokutoa, wengine baba zao mafisadi wanawatafutia watoto wao nafasi nzuri Serikalini na ktk makampuni binafsi au wengine wanakuta kila kitu kipo tayari akifika 22 to 30 then basi anapewa mtaji wa kuanzia.
Ata mkisema alichukua mkopo Bank basi utakuta alimpa Branch Manager na wanaohusika kutoa mikopo rushwa na kuchukua mkopo wa milioni 500 bond aliweka nyumba ya Baba yake aliyopata kwa ufisadi.
Wewe fikiria mimi Chimwaga Baba na Mama yangu ni masikini wa kutupwa, Nimesoma shule ya msingi Mianzini, Sekondari Tambaza, Chuo kwa shida UDSM, mshahara baada ya kodi 850,000 au 900,000 familia yangu watoto wawili, wadogo zangu 3, Baba na Mama, Ukoo wangu bila ya kuwasahau mke wangu na ukoo wake ambao wote ni Masikini wa kutupwa hivi tunaweza kutoka kwa Tsh 900,000 kama sijaanza ya kuwa fisadi au mwizi wa kutupwa ofisini kwangu? Na siwezi kuwaacha hawa wote kwakuwa ni familia yangu au wengine walinisaidia wakati nasoma, nk.
Kwa ufupi wote waliotoka wakiwa na miaka 40 wamshukuru Mungu na ufisadi wao au wa Baba zao ila isiwe kejeri kwa wasiotoka, na kama hii makala ni ya kuwatia moyo wasiotoka basi ni sawa sawa na stori alizozitoa Kinjeketile wakati wa vita ya maji maji!
Kutoka kwa mtu hakujali umri wala wakati. Binadamu wote hatulingani na tunaanzia maisha kwenye mazingira tofauti. Uwezi kufanya kila mtu afanikiwe katika maisha eti kabla ya miaka 40. Mimi nitamfurahia mtu aliyefanikiwa akiwa na miaka 60 kwa kutumia ujuzi wake na juhudi zake kulikoni aliyefanikiwa akiwa na miaka 30 kwa dhuluma.
ReplyDeleteSI waelewei naona kama wote mnaondika hapa wanaume!Mi nina 35nina nyumba nina gari ya kawaida tu mtotoanaweza kwenda shule ya mil. 7 kwa mwaka sasa bado naona sijatoka kwamba pamoja na kuajiriwa na kujiajiri mama yangu hajakaa maisha ninayoyataka mimi mwenyewe sijui kama nataka kukaa kwenye nyumba na nusu heka! Nina heka tano kibaha lakini ramani ni nyumba ninayotaka siwezi ku'afford; Manaongea nini? "Kutoka" kuna maana gani kwenu?
ReplyDeleteMkuu wa mkoa wa naniiii tunakuomba uirudie tena hii mada kwa kuiweka juu zaidi.
ReplyDeleteTajiri anatoka kwa dhuluma aka ufisadi aka Rushwa, Masikini anatoka baada ya kwenda Mlingotini.
ReplyDeleteAta Mafisadi siku hizi nasikia wanatinga Mlingotini kwa jinsi wasivyorizika na walichonacho.