I:UTANGULIZI 
                                 
a)Masuala ya jumla

Mheshimiwa Spika,
1. Leo tunahitimisha shughuli za Mkutano wa Kumi na Sita na Kumi na Saba wa Bunge lako Tukufu.  Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.

Mheshimiwa Spika,
2. Mkutano huu ulijumuisha kujadili kazi kubwa zifuatazo:

Kwanza: Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2015/2016;

Pili:Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014 [The Tax Administration Bill, 2014];

Tatu:Muswada wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani wa Mwaka 2014 [The Value Added Tax Bill, 2014];

Nne:Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2014 [The Public Private Partnership (Amendment) Bill, 2014]; na
Tano:             Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa Mwaka 2014, [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2014].

Aidha, ni hivi mapema leo Miswada 11 ya Sheria ya Serikali kuhusu mambo mbalimbali ilisomwa kwa mara ya kwanza.

Kusoma hotuba kamili BOFYA HAPA

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi (kushoto) wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Bungeni mjini Dodoma leo Novemba 29, 2014

 Mawaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya  (kulia) na Stephen Wasira  (kushoto) wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bugeni, Freeman Mbowe, Bungeni mjini Dodoma leo Novemba 29, 2014. 
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya (kulia) akizungumza na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mjini Dodoma Novemba 29, 2014. 
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya wabunge, Bungeni mjini Dodoma Novemba 29, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu n Mafunzo ya Ufundi. Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Michuzi nakuheshimu sana...lakini unapoacha kuandika yale aliyosema waziri mkuu kuhusu Escrow kwenye hiyo hotuba uliyo-post, inanitia shaka...

    Naanza kujiuliza maswali mengi, kwa nini issue nyingine zote umeandika kwa kina lakini ilipofika Escrow you just wrote one sentence!!!

    There is a lot hidden here....maazimio ya Bunge yamefanyika lakini hakika Mungu atatulipia hayo yote yaliyokufanya ushindwe kupost full story.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...