![]()
Inaniwia vingumu sana kutoa shukrani kwa mtu mmoja mmoja au makundi kutokana na ushirikiano wenu katika kipindi kigumu cha msiba na mazishi ya mpendwa mume wangu na mwenyekiti wa Dorka catering na Dorka group of company
Marehemu Dr kephas kansolele Ntevi.
Kwa niaba ya familia yangu napenda kutoa shukrani za dhati kwa wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine kwa kipindi chote cha msiba wa mume wangu. Kiukweli tulipatwa na kigugumizi ambacho hakisemeki Ingawa nyote mnastahili kushukuriwa lakini ningependa kutoa shukrani zangu za pekee kushukuru madaktari wa Muhimbili na manesi kwenye kitengo cha I.C.U. Dr Kalianyama mlifanya kazi usiku na mchana kuokoa maisha ya mume wangu lakini mungu alimpenda zaidi Kanisa la Good News Mission Tanzania Pastor kiongozi Jeong na ma-pastor na waumini wote hamkuchoka kutuombea na bado mnatuombea tuna shukuru sana Service Provider wezangu kiukweli mmenionyesha upendo ambao hausemeki, Marafiki zangu na wa familia mlikua na sisi usiku na mchana hamkutuacha. Networks wote waliokua wana shirikiana na mume wangu.
Blogs mbalimbali, majirani zetu wa mwenge na Bahari beach , Familia ya Ntevi, Familia ya Wakaombwe na ya Mzee Massau tunapenda kuwashkuru wote kwa upendo na faraja zenu
Sina maneno mazuri ya kuonyesha shukurani zetu za dhati kwa niaba yangu na wanangu, tunaomba mpokee shukurani zetu mwenyezi mungu awaongezee pale mlipo toa.
Tutakua na Ibada ya shukurani nyumbani kwa marehemu kunduchi njia panda ya madini. Ratiba itakua kama ifuatavyo
Tarehe 5/12/2014 mkesha Ibada na dinner (BBQ Night)
Tarehe 6/12/2014 kuanzia saa 2 asubuhi wageni kuwasili na saa nne (BRUNCH) Hadi saa tano mchungani wa Good News mission atapowasili na saa tano na nusu ibada neno la shukrani ya familia
kwa mawasiliano ::+255718 661 705 / +255717 056 598
Bwana ametoa na Bwana ametwaa.
Wote mnakaribishwa kushirikiana
na sisi kumtolea Mungu shukrani |
Home
Unlabelled
IBADA YA SHUKRANI za dhati kwenda kwa wadau wote
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...