Hali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alifanyiwa operesheni Jumamosi, inaendelea kuimarika na kuwa nzuri na jana, Jumapili, Novemba 9, 2014, alianza kufanya mazoezi ya kutembea.

Rais Kikwete ameanza kufanya mazoezi ya kutembea siku ya pili tu baada ya kufanyiwa operesheni ya tezi dume (prostrate) kwenye Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Maryland, Marekani.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, itaendelea kuwapatia wananchi habari sahihi kuhusu maendeleo ya afya ya Mheshimiwa Kikwete kwa kadri habari hizo zitakavyokuwa zinapatikana.

Aidha, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kuwashukuru sana wote ambao wamekuwa wakimwombea Rais Kikwete, ili apone haraka na kurejea nyumbani kujiunga na wananchi wenzake katika ujenzi wa taifa letu. Tunawaomba waendelee kumwombea.
Pichani anaonekana Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula akimjulia hali Mhe Rais.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

10 Novemba,2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Tunamtakia rais wetu afya njema na uponaji wa haraka.
    Tunaomba pia hosipitali zetu za rufaa ziimarishwe ili matibabu kama haya yafanyike nyumbani.

    ReplyDelete

  2. Ameen In Sha Allah itakua kheri mola atamponya haraka.

    Chef, Sweden

    ReplyDelete
  3. Pole sana baba yetu, Mungu yu pamoja nawe tunakuombea afya njema mpendwa wetu na baba yetu.

    ReplyDelete
  4. Ninashukuru kusikia rais wetu anaendelea vizuri. Ombi langu moja kwa mheshimiwa rais, Ukirudi nyumbani ufanye taratibu za matibabu kama haya yaweze kuwa ya uhakika kufanyika huko nyumbani, ni aibu watanzania wengi kufa kwa magonjwa yanayotibika. Hospitali zetu zote za mikoa ziwezeshwe kufanya upasuaji kama huu ili tuokoe maisha ya watanzania maskini ambao ndiyo wengi.

    ReplyDelete
  5. Get well soon Mr.President
    May the Almighty grants you quick recovery.Our prayers are with at this time

    ReplyDelete
  6. TUNAMTAKIA RAIS DR. JM KIKWETE AFYA NJEMA, APATE KUPONA MAPEMA NA AREJEE NYUMBANI SALAMA ILI AENDELEE NA KAZI ZAKE ZA UJENZI WA TAIFA. AMINA.

    ReplyDelete
  7. Pole Rais wetu mpendwa Mungu akujalie upone haraka, Mimi na familia yangu tunakutakia afya njema.

    ReplyDelete
  8. Pole sana Rais wetu Mungu akujalie upate nguvu mapema uweze kurudi nyumbani. Na nashukuru sana Balozi wetu mpendwa kwa kumjulia hali na uendelee na roho hiyo hiyo ya upendo kama ulionao mama

    ReplyDelete
  9. GET WELL SOON MZEE WA MSOGA! WE LOVE YOU

    ReplyDelete
  10. ugua pole Rais wetu.
    jamani mtu yuko hospitali mnapa orodha ya majukumu? subiri apone mtoe maoni ya kuhimarisha matibabu Bongo.
    Hata huku bima za hospitali ukiwa nayo unaruhusuiwa kutibiwa nje kama hu ogonjwa una hosptali iliyo na ubingwa zaidi nje ya nchi, kwa hiyo sio kero viongozi au watu binafis kutibiwa India au marekani.tusiwe na mwelekeo wa kulaumu, hata mtu akiwa kitandani! wabongo tumezidi kulaumu..
    NB: Mwisho nimefurahi kuona kwa mara ya kwanza maoni yote hakuna mashambulizi maklai kama ambayo nimekuwa nayasoma kuhusu utendaji wa huyu Rais wetu..mazuri watu hwayaoni kama barabara nchi nzima..umeme vijijini nk..kazi ameifanya na hawezi kumaliza matatizo yote kwa vipindi viwili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tunampa pole rais wetu...kuna shida gani kumkumbusha awasaidie watanzania wengine wengi wwnye matatizo yenye kuhitaji surgery? Hata tukimweleza hapa si analo jukumu la kuwafahamisha na kuwakumbusha walio chini yake? Hapa sioni shida. Wewe unaongelea barabara na umeme wa mgawo wakati wote hapa wanazungumzia huduma za afya ambazo si nzuri au ni kwa watu wachache, wewe anon wa hapo juu kumbuka ni haki ya watanzania wote kupata huduma kumbuka pia hatuongelei mengine unayoyofikiria.....kama ni barabara, maji, umeme n.k ni haki yetu wananchi wote kuwa na access nayo.

      Delete
  11. Tunakutakia uponyaji wa haraka.

    ReplyDelete
  12. Mhe Rais,

    Your well being means a lot to us.We pray for you.

    Get well soon.

    Saidi Yakubu
    Dar

    ReplyDelete
  13. Get well soon Dady.. We love you!!!

    ReplyDelete
  14. Tunamtakia rais wetu afya njema na uponaji wa haraka.

    ReplyDelete
  15. Ugua pole Mheshimiwa Rais wetu, tunakuombea upone haraka na urejee nyumbani kuendelea na majukumu yako.

    ReplyDelete
  16. Pole sana Mheshimiwa Rais wetu tukupendaye Dr Jakaya Mrisho Kikwete. Mwenyezi Mungu akupe ahueni ya haraka na urudi nyumbani Tanzania salama uendelee kutuongoza. Watanzania wote tukupendao tunakuombea kwa M/Mungu upone haraka.

    Peters Mhoja - Sweden

    ReplyDelete
  17. Nakuombea Mungu Rais wetu Mpendwa, Mungu akuponye haraka sana na akupe nguvu afya njema ili uweze kurudi nyumbani na undelee na majukumu yako ya kuongoza Taifa letu. Ameen

    ReplyDelete
  18. Wish you WELL Mr President. Love you!!😆😆😆

    ReplyDelete
  19. MR PRESIDENT our country,, is with you. Get WELL''

    ReplyDelete
  20. Mr President get well soon. Mungu akupe afya. PIA NASHUKURU KWA KUTUFUMBUA MACHO KUHUSU UGONJWA HUU? WANAUME WENGI TUNAJIFICHA!,UNGEWEZA KUTIBIWA KIMYAKIMYA TUSIJUE LAKINI KWA KUWA WAZI KATIKA HILI NAAMINI WATANZANIA WENGI WATAPONYWA KWA KUPATA UELEWA

    ReplyDelete
  21. Pole sana Rais wetu, Bwana Yesu akuponye, akulinde na akupe afya njema urudi kuliendeleza taifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...