Na Teresia Mhagama
Kamishna wa madini nchini, Mhandisi Paul Masanja amefungua rasmi mafunzo ya uongezaji thamani madini kwa wanawake 15 wa kitanzania waliopata ufadhili wa masomo hayo ambayo ni matunda ya harambee iliyoanzishwa na Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha mwaka 2012.
Mafunzo hayo ya ukataji madini yatakayowawezesha wanafunzi husika kukata madini na kuyachonga katika maumbile ya kuvutia yatakuwa yakitolewa kwa muda wa miezi Sita katika Kituo cha Jimolojia (TGC) kilichopo jijini Arusha ambacho kipo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.
Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul
Masanja (wa tatu kutoka kulia) akizungumza na mmoja wa wanafunzi waliopata
ufadhili wa masomo ya uongezaji thamani madini yanayoendeshwa katika Kituo cha
Jimolojia (TGC) jijini Arusha, wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Ushauri wa Madini nchini, Richard Kasesela (wa nne kutoka kulia), Meneja wa
Uthaminishaji Madini kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA), George
Kaseza (wa pili kutoka kulia) na Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra
Masoud (wa kwanza kulia).
Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul
Masanja (wa nne kutoka kushoto mstari wa pili) akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi 15 waliopata ufadhili wa masomo ya uongezaji thamani madini yanayoendeshwa
katika Kituo cha Jimolojia (TGC) jijini Arusha. Wengine katika picha ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini nchini, Richard Kasesera (wa pili
kushoto mstari wa pili),Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini
nchini (TAMIDA), Sammy Mollel (wa tatu
kushoto mstari wa pili),Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya
Kimataifa ya Vito Arusha, (AGF), Peter Pereirra(wa tatu kulia mstari wa pili)
Mwalimu anayefundisha masomo hayo kutoka nchini Sri Lanka, Pathmasiri Alwis (wa kwanza kushoto mstari wa pili) pamoja
na watendaji Kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Kituo cha Jimolojia (TGC) na
Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA).
Baadhi ya wanafunzi waliopata ufadhili wa
masomo ya uongezaji thamani madini wakionesha baadhi ya madini ya vito ambayo
yamekatwa na kuchongwa katika maumbo ya kuvutia baada ya kupata elimu hiyo
kutoka kwa mwalimu Pathmasiri Alwis wa nchini Sri Lanka. Pamoja nao ni Kamishna
wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja ( wa pili kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya
Ushauri wa Madini nchini, Richard Kasesela (wa kwanza kushoto),Mwenyekiti wa
Chama cha Wafanyabiashara wa Madini nchini (TAMIDA), Sammy Mollel (wa pili kushoto),Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Vito Arusha, (AGF), Peter
Pereirra(wa kwanza kulia mstari wa pili)
Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane akiangalia jinsi wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya
uongezaji thamani madini wakichonga
madini ya vito katika maumbo ya kuvutia katika Kituo cha Jimolojia (TGC) Arusha
kilicho chini ya Wizara ya Nishati na Madini.
Mmoja wa wanafunzi waliopata ufadhili wa
masomo ya uongezaji thamani madini akijifunza
kuchonga madini ya vito ili yawe katika umbo la kuvutia kabla ya kumfikia mtumiaji.
safi sana, better late than never. Sasa bado the first of its kind duty free jewelry mall ili tuuze vito na dhahabu zilizoongezwa thamani.
ReplyDelete