Kampuni ya Bima ya Resolution leo hii imeaanda siku maalum ya familia kwa ajili ya wateja wake katika viwanya vya Posta jijini Dar es Salaam.

Hii ni mara ya kwanza kampuni hiyo imeaanda siku hii maalum kwa ajili ya wateja wake na kulikuwa na burudani ya kutosha kutoka bendi ya Borabora, DJ maalum na vichekesho kutoka MC Pilipili. Kulikuwa pia na michezo mbalimbali ya watu wazima na watoto kama vile: soka, dance limbo na tug of war. Wateja waalikwa walipata chakula kwani kulikuwa na chakula cha kutosha.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution Bwana Oscar Osir alisema, “ Tukiwa tunaelekea kumaliza mwaka wa 2014 tuliona muhimu kumaliza mwaka kwa furaha na ndio maana tumejumuika na wateja wetu leo katika siku hii ya familia

“ Kadri kampuni yetu inavyozidi kukua mchini Tanzania tunatarajia kuwa na siku maalum zingine kama hizi ili kufurahi pamoja na wateja wetu. Wateja wetu wametuamini kuwapa bima ya afya bora na kwa familia zao na hivyo basi ni vizuri kuwaonyesha jinsi tunavyowathamini” Bwana Osir alisema

Kampuni hiyo pia ilitoa huduma ya afya na kuwapa wateja wao fursa ya kujadiliana maswala tofauti ya afya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Resolution Insurance, Oscar Osir (kushoto)akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya Wanafamilia wa kampuni hiyo iliyofanyika mwiashoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Kulia ni Watoto wa wakisubili keki ikatwe wale.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Resolution Insurance, Oscar Osir(katikati) akikata keki wakati wa hafla ya kampuni hiyo kwa wafanyakazi na wateja iliyofanyika Viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam.
Mchezaji Abdalah Abdul(kulia) akijaribu kumtoka Hilari Salehe wakati wa hafla kwa nafamilia wa Resolution Insurance(Bima ya Afya) iliyofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi zya washiriki wa mbio za Magunia wakishindana wakati wa wa hafla kwa nafamilia wa Resolution Insurance(Bima ya Afya) iliyofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Robert Kishiki alishinda mbio hizo.
Wafanyakazi wa Resolution Insurance wakiwaburuza wateja wakati wa mpambano wa kuvuta kamaba baina ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wateja uliofanyika viwanja vya kijitonyama jijini Dar es Salaam mwioshoni mwa wiki.Wafanyakazi wa Resolution Insurance walishinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...