Taasisi isiyo ya kiserikali inayo shughulika na uhifadhi wa mazingira eneo la Kinukamori, Marangu mkoani Kilimanjaro Executive Wilderness Program (EWP) inatafuta dola za marekani 30,000 kwa ajili ya kuendesha program tatu zenye kutengeneza ajira, ujasirimali, utunzaji wa mazingira na mvuto kwa watalii wanaokwenda kupanda mlima Kilimanjaro.

Kauli hiyo wameitoa kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez wakati alipofanya ziara mkoani Kilimanjaro kuangalia miradi inayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Uongozi wa EWP and Kinukamori Enterprises katika taarifa yao kwa Mratibu huyo, iliyosomwa na Mshauri wao wa fedha Grace Shayo wamesema pamoja na nia yao ya kuhakikisha maporomoko ya Kinukamori yanaendelea, kwanza kama taasisi na pili kama mradi wa kuhifadhi mazingira ya Mlima Kilimanjaro ambao ni sehemu ya urithi wa dunia, wakishirikiana na KINAPA wamefikiria miradi kadhaa ambayo ikienda kwa pamoja itaendeleza eneo hilo.

Wamesema fedha hizo zitatumika kutoa elimu ya ujasirimali kwa vijana 300 wanaoishi katika jamii ya Marangu ambao hutoa huduma mbalimbali kwa wenyeji na pia wageni wakiwemo watalii. Kundi hilo linalotakiwa kupewa mafunzo ni pamoja na wapagazi 50, waendesha pikipiki 100, wachuuzi 100 na walima mboga 50.
DSC_0218
Mkurugenzi Mtendaji wa EWP na Mkurugenzi wa Kinukamori Enterprises, Bw. Alpha Phares Moshi (wa pili kushoto) akimkaribisha Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez alipowasili kwenye Taasisi isiyo ya kiserikali inayo shughulika na uhifadhi wa mazingira eneo la Kinukamori, Marangu mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na UNDP huku akiwa amembatana na Mratibu wa Kitaifa miradi ya COMPACT mkoani Kilimanjaro, Victoria Nderumaki (wa tatu kulia) pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (wa pili kushoto).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...