Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij keshokutwa (Novemba 5 mwaka huu) atatangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itakayochezwa ugenini Novemba 16 mwaka huu.
Nooij atatangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari katika mkutano utakaofanyika saa 4.30 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko ghorofa ya tatu, Jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Swaziland, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Mbabane.
hivi hawa expert waakuja kufanya nini kama Tz haijawahi hata kunusa harufu ya kombe la dunia?
ReplyDeleteKaka wewe angalia tu halafu mezea kwani hata historia ya timu yetu ya Taifa kwanza hatuijui ila tu na sikia timu yetu ili fuzu kwa fainali Za kombe la bara Kabla hata sija zaliwa... Tangu hapo mpaka leo hata hatua ya mzunguko hatumalizi Msumbiji nao hata Huluma hawatuonei....sina mengi ya kusema ila kama tuna taka soccer basi tuanzie na uongozi wote kupiga nyama chini... Halafu
ReplyDelete