Baada ya Mwezi Oktoba kuisha ambapo kubwa lilikua ni kukuza uelewa juu ya matumizi salama ya mitandao, Taarifa ya kumalizika kwa mwezi huo inaweza kusomeka"HAPA" Mambo mengi tuliyo yajadili yameonekana kuangaziwa tena kwenye kongamano la maswala ya TEHAMA Jijini Cairo Nchini Misri. Muundo wa kongamano hili ulihusisha meza kuu inayo fungua mijadala na wasikilizaji kuchangia na kuuliza mwaswali pamoja na kupata njia ya kufikia malengo kupitia mada tofauti tofauti.

Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba, Katika Meza kuu ya Mjadala alio husisshwa alipata kuzungumzia jinsi teknolojia ya habari na mawasiliano inavyo patiwa kipaumbele cha mwishoni na idara za fedha katika mataifa mbali mbali ingawa ni sekta ambayo ina nafasi kubwa sana katika kuleta mabadiliko na kukuza kwa haraka uchumi wan chi yeyote kama itatumika vizuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...