DONATA GASPAR TARIMO:
7/8/1958 - 31/10/2013
Mama, ni mwaka mmoja sasa tangu ulivyoitwa na Bwana Mungu siku ile ya tarehe 31 Oktoba, 2013 saa Nne usiku. Kimwili hauko nasi, lakini kiroho tunaamini upo nasi. Daima tunakukumbuka mama, kwa upendo wako, ukarimu, ucheshi, busara zako, ushauri wako kwetu na kwa kuleta mshikamano katika familia.
Mama, ulikua nguzo muhimu katika kuhimili mawimbi na kustawisha maendeleo katika familia na jamii inayotuzunguka. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa muda wote tuliokuwa na wewe hapa duniani, kwani malezi yako mema yamekua msingi mkuu wa maisha yetu. Tunaamini siku moja tutakutana huko uliko mama.
Ingawa maisha yanaendelea, tunakosa mengi sana tuliyoyazoea kutoka kwako na hatuwezi kufananisha hali ilivyo sasa hata chembe na namna tulivyokuwa na wewe. Tulikupenda sana mama, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Unakumbukwa sana na mumeo Gaspar, wanao Martha, Michael, Kuki-Renatus, Charles na Emmanuel. Mkweo Jackline, na mjukuu wako Lance-Manase. Unakumbukwa pia na mama yako, kaka zako, dada zako, shemeji zako, wifi zako, wapwa zako, ndugu zako, majirani, jamaa na marafiki.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho yako mahali Pema Peponi. Amina.
….Mimi ndimi ufufuo na uzima, yeye aniaminiye ajapo kufa, atakuwa anaishi, nae kila aishie na kuniamini hatakufa kabisa hata milele……
Yoh 11: 25-26
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...