Walimu (ma-Sensei) watano toka Tanzania, yaani Sensei
Dudley Mawalla, Sensei Daud Magoma, Sensei Kheri Kivuli,
Sensei Edgar Kaliboti na Sensei Rumadha Fundi, wanatoa shukrani nyingi sana kwa kupewa dhamana kubwa ya heshima na vyeo vya
ngazi za juu toka shirikisho la Karate Tanzania (Tanzania
Karate-Do Federation).
Chini ya uongozi wa mwenyekiti Sensei Geofrey Kalonga na
katibu mkuu wake Sensei Phillip Chikoko, wana-sema ma-Sensei hao katika waraka ulioandikwa na Sensei Rumadha Fundi kwa niaba ya wote kuwa wao hawana budi
kuitikia wito wa kuchangia maendeleo ya sanaa ya Karate
inayohitaji nidhamu na mifano ya ujasiri wa hali ya juu
kwenye kizazi kipya cha taifa letu.
Sensei Dudley Mawalla na Sensei Daudi Magoma, walitunukiwa
shahada au Dan ya Saba kila mmoja, wakati Sensei Kheri Kivuli, Sensei
Kaliboti na Sensei Rumadha Dan sita kila mmoja.
Sensei Dudley
Mawalla, mwanzilishi wa Japan Shotokan Tanzania. Sensei
Kaliboti, mkufunzi wa Gracie Ju jitsu, Australia, Sensei
Rumadha, Okinawan Goju Ryu Jundokan KyoKai, Texas, USA,
Sensei Daudi na Sensei Kivuli, wakufunzi wa Okinawa Goju
Ryu, Dar Es Salaam, Tanzania.
Sherehe hizo zilifanyika uwanja wa ndani wa taifa
kuadhimisha siku ya baba wa taifa Mwalimu Nyerere,
kushirikishwa na zaidi ya wana-Karate 50 wa ngazi mbalimbali
toka shule na mikoa tofauti hapa nchini.
"Wote tuliotunukiwa
heshima hiyo, hatunabudi kusema asante zetu katika
shirikisho la Karate Tanzania(Tanzania Karate-Do
Federation", unamalizia waraka huo ambao Globu ya Jamii ina nakala yake
Katibu Mkuu wa Tanzania Karate Do Association Sensei Philip Chikoko (kushoto) akimtunuku Sensei daudi Magoma shahada au Dan ya Saba
Katibu Mkuu wa Tanzania Karate Do Association Sensei Philip Chikoko (kulia) akimtunuku Sensei Kheri Kivuli shahada au Dan ya Sita
Sensei Edgar Kaliboti akiwa anasimamia mafunzo ya mtindo wa Gracie Ju jitsu huko Australia. Tanzania Karate do federation imemtunuku Dan ya sita
Sensei Dudley Mawalla akitunukiwa Dan ya saba na Mwenyekiti wa Tanzania Karate do Federation Sensei Godfrey Kalonga (kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Karate Do Association Sensei Philip Chikoko
Sensei Rumadha Fundi akicheza kata. Yeye ametunukiwa Dan ya Sita
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...