Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bwana Kyle
Peters amefanya ziara katika kijiji cha Buma wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani
ambako ameshuhudia walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na
TASAF na kuridhishwa kwake na namna mpango huo ulivyowanufaisha walengwa ambao
wameanza kuondokana na umaskini.
Akiwa kijijini hapo Bwana Peters alitembelea
moja ya nyumba iliyoboreshwa na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya
maskini Bwana Bakari Rajabu Bakari ambaye kwa kutumia fedha za ruzuku kupitia
Mpango wa kunusuru kaya maskini ameweza kuboresha maisha yake ikiwa ni pamoja
na kununua Luninga(TV) huku akimudu pia kusomesha watoto wake.
Bwana Peters amesema utekelezaji wa Mpango
huo umeanza kuonyesha mafanikio nchini TANZANIA
jambo ambalo litatumiwa na Benki ya Dunia kuendelea kuufadhili huku
mfano huo ukisambazwa katika nchi nyingine ili kazi ya kuutokomeza umaskini iwe
na mafanikio.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema mafanikio ya utekelezaji wa
Mpango wa kunusuru kaya maskini yanatokana na taasisi yake kuamini na
kutekeleza majukumu yake kwa uwazi na kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo
walengwa katika hatua za utekelezaji wake.
Zifuatazo hapo chini ni baadhi ya picha za
ziara ya makau huyo wa Rais wa Benki ya Dunia katika kijiji cha Buma wilaya ya
Bagamoyo mkoani Pwani.
Makamu wa Rais wa Benki ya
Dunia Kyle Peters akiwahutubia wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini
katika kijiji cha Buma wilayani Bagamoyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF
Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa masuala ya mpango wa
kunusuru kaya masikini kwa walengwa (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Makamu
wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters.
0Baadhi ya wanuafaika wa mpango
wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF
katika kijiji cha Buma wilyani Bagamoyo wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu
wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus
Mwamanga.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo
Ahmed Kipozi akimkaribisha Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters
alipotembelea miradi ya TASAF wilayani humo. Kushoto kwake Mkurugenzi Mtendaji
wa TASAF Ladislaus Mwamanga.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...