Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb) akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Bunge leo na kuainisha hatua madhubuti za kuchukuliwa na serikali ili kukomesha mauaji baina ya wakulima na wafugaji yanayoendelea Mkoani Manyara wilaya Kiteto na sehemu nyingine nchini.
Wajumba wa Kamati ya Uongozi ya Bunge wakimsikiliza Waziri Mkuu kwa umakini mkubwa alipokuwa akitanabaisha jinsi Serikali isivyopendezwa na mauaji ya Kiteto na jinsi ilivyojipanga kukomesha kabisa mauji hayo.
Naibu Spika na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwa jinsi walivyozungumza na Mhe, Waziri Mkuu kwa moyo wa kizalendo kwa nchi yao.
Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah (kushoto) akitoa ushauri kwenye Kamati ya Uongozi jinsi ya kuwasilishwa Bungeni taarifa za Tume mbalimbali leo.
Picha na Prosper Minja-Bunge
Serikali inatakiwa kuwa na sera ya ardhi, bahari na maziwa ya maji baridi.
ReplyDeleteSera ya ardhi ilenge kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ukulima na pia maeneo maalum kwa ajili ya ufugaji.
Sera ya bahari ilenge kuwabana washimbaji mafuta na gesi kutochafua bahari ili wavuvi waendelee na shughuli zao za kujipatia kipato.
Sera ya maziwa ya maji baridi kama ziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa n.k ili kulinda mazingira ya maziwa hayo na kuwawezesha wananchi wanaotumia maziwa hayo kuweza kujipatia kipato.
Haya matamko bila sera madhubuti za Ardhi, Bahari, Maziwa kuratibiwa kuanzia serikali kuu, serikali za mkoa, halmashauri za wilaya na vijiji hayataweza kutatua tatizo la wananchi kugombania rasilimali hizo.
Maana idadi ya watu inaongezeka na hivyo wananchi hawawezi kuachiwa kufanya shughuli zao za kujipatia kipato kiholela holela bila sera nzuri itakayowaongoza wapi wajenge nyumba, wapi wafanye shughuli ya ukulima, ufugaji, uvuvi, madini n.k
Serikali lazima ijifunze kutoka ktk historia za mapigano ya kugombea ardhi, bahari n.k maana mambo haya yanajirudia rudia lakini somo la historia linadharaulika ktk kusaidia kuondoa tatizo hili.
Na masuala haya lazima yaingizwe kwenye Katiba.
Mdau
Maono ya Historia
Serikali hii ya Raisi Kikwete na Waziri mkuu Pinda imekuwa na uongozi ambao badala ya kuongoza wanalalamika na kulaumu kwamba hakuna uongozi. Hotuba ya raisi Kikwete kwenye ufunguzi wa barabara ya Bagamoyo alisikikika anasema kwamba kushindwa kusimamia miundombinu ya barabara inatokana na uongozi mbaya. Sasa, kiongozi ni nani anayelaumiwa. Ni kama vile baba analaani usimamizi mbaya ndani ya nyumba yake. Mhariri wa the Guardian alisema tunachohitaji ni vitendo na wala sio Malalamiko. Hii nchi yetu ya Tanzania tumelala, viongozi wetu ndio kabisa wamelala fofofo. Inabidi tuamke, vinginevyo hata nchi tu za jirani wanatuacha mbali.
ReplyDeleteNakubaliana na wewe mdau wa hapo juu. Hili ni suala la kisera ambapo hufuatiwa na kuweka sheria madhubuti ambapo kila mtu atakua mipaka yake
ReplyDelete