![]() |
Mbunge Ritta Kabati |
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) amewakata wananchi kutokubali kudanganywa na vyama vya siasa vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) juu ya mchakato wa katiba iliyopenekeshwa na badala yake kuungana na watanzania wapenda maendeleo kuikubali katiba hiyo muda utakapofika.
Mbuge Kabati alitoa kauli hiyo kwa nayakati tofauti juzi na jana wakati wa semina zake za ndani na wanawake wanachama wa UWT katika wilaya ya Iringa , Kilolo na Mufindi semina iliyolega kuwajengea uwezo wa kujiamini kwa wanawake waliojitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uongozi wa serikali za mitaa na vijijini .
" Mimi kama mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa wajibu wangu ni pamoja na kukutana na wananchi wa Iringa na kuwajengea uelewa mpana wa katiba hiyo iliyopendekezwa ila muda ukifika wa serikali kutangaza mchahato wa kupokea maoni ya wananchi juu ya katiba hiyo iliyopendekezwa basi viongozi hao waweze kuelewa zaidi pamoja na wananchi wanaowazunguka..... hivyo nitaendelea kutoa elimu kwa viongozi wa chama katika semina mbali mbali"
Kabati alisema kumekuwepo na upotoshwaji mkubwa ambao umeendelea kufanywa na UKAWA kwa kuzunguka huku na kule kujaribu kupotosha ukweli juu ya katiba iliyopendekezwa kwa madai kuwa ni katiba ya CCM jambo ambalo ni upotoshaji mkubwa na kuwa mchakato wa katiba hiyo ulifanywa na vyama vyote na makundi maalum.
Pia alisema kuwa kitendo cha baadhi ya wanasiasa wasilolitakia mema Taifa hili kwa kupotosha juu ya katiba hiyo ni sawa na kutaka kuona nchi haitawaliki na hivyo kuamua kuanza upotoshaji huo.
Alisema kuwa si kweli kama katiba hiyo iliyopendekezwa haina jambo lolote la msingi kama ambavyo UKAWA wamekuwa wakizunguka na kupotosha ila alidai kuwa ndani ya katiba hiyo kuna mambo mengi yamezingatiwa kwa ajili ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Akielezea kuhusu mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ,vijiji na vitongoji unaotaraji kufanyika hivi karibuni alisema kuwa upande wa mkoa wa Iringa wanawake baada ya kuhamasishwa wamepatika kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania nafasi mbali mbali za uongozi na kuwa baadhi ya maeneo wamepata kushinda kwa kishindo nafasi walivyoomba ndani ya CCM wakisubiri uchaguzi rasmi wa serikali .
Hivyo aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kujitokeza kuwapa kura zao wanawake hao waliogombea nafasi mbali mbali na kuwa imani yake kuona kunakuwa na uongozi mchanganyiko.
Hapa ndipo tunapojichanganya! Kukubali nini wakati bado hatujaisoma na kujulishwa au kuelimishwa kuhusu kilichoandikwa? Kama sio "rubber stamp" ni nini?
ReplyDeleteKwani ukawa wanapowambia muikatae mmeisoma....?
ReplyDelete