
Lengo ni kutoa fursa kwa washiriki wa mdahalo na wananchi kwa ujumla kujielimisha kuhusu Katiba inayopendekezwa ili waweze kuielewa vizuri, na hivyo kujiandaa kuipigia kura katika mazingira ya uelewa kwa kuzingatia dhamira yao, bila kulazimishwa, kutishiwa au hata kulipwa fedha na mtu au kundi lolote. Hakuna kiingilio katika mdahalo huo, na watu wote wanakaribishwa.
Mdahalo utafanyika kati ya saa 9.00 mchana na saa 12.00 jioni kwenye Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza, Dar es Salaam. Washiriki wote wawe wamefika Blue Pearl Hoteli saa 8 mchana.
2. Washiriki katika mdahalo huo ni baadhi ya waliokuwa Makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wakiwamo Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph S. Warioba, Mzee Joseph W. Butiku, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bibi Mwantumu Malale, Mtumishi wa Umma Mwandamizi Mstaafu, ,
Ndugu Awadh Ali Saidi, Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar na Ndugu Humphrey Polepole, Mdau wa Maendeleo), Profesa Baregu, Jaji Mstaafu Mzee Ussi (Zanzibar) na Ndugu Muhammad Mshamba (Zanzibar).wananchi na viongozi kutoka taasisi na asasi mbalimbali. zinazowakilisha jamii ya Watanzania ambazo ni pamoja na asasi za kiraia (NGOs), vyama vya siasa, madhehebu ya dini, wasomi, vyombo vya habari, taasisi za kitaaluma, vyama vya ushirika vya wakulima na wafugaji, vyama vya wafanyakazi, n.k. wanakaribishwa kushiriki.
3. Mdahalo utarushwa moja kwa moja na ITV. Kwa kupitia TV na Redio zao na TV Sibuka Maisha. Wananchi po pote walipo wanaombwa kushiriki katika mdahalo huo.
Imetolewa na:
Mkurugezi Mtendaji,
Taasisi ya Mwalimu Nyerere,
S.L.P. 71000,
Fax No. : 255 22 2119216/2118354
Email: info@nyererefoundation.org
India/Makunganya/Bridge Street
1 Novemba, 2014
Msaada ankal, hivi neno "mdahalo" maana yake ni nini? uwelewa wangu ni majadiliano ya pande zenye mitazamo tofauti juu ya suala husika. Hivi hili kundi lenye mtazamo mmoja ng'ang'anizi wataweza kuwa na mdahalo? hapa ni maoni ya kundi fulani juu ya katiba inayopendekezwa. Mstarabu wa kweli hanabudi kuheshimu mawazo mbadala hata kama hakubaliani nayo. Ukabaila utalimaliza Taifa letu ni lazima tuwe makini na watu wa aina hiyo.
ReplyDelete