Andrew Chale (kulia) akiteta jambo na 'Mwenyekiti' Maggid Mjengwa wa Mjengwa Blog. ..
Ni vya 'Who Is Andrew Chale', 'Nimnukuu Nani?' na ''Mimi ni Historia',
Mwandishi
wa Habari nchini Tanzania, Andrew Chale anayeandikia magazeti ya
Tanzania Daima na Sayari yanayotolewa na kampuni ya Free Media ya jijini
Dar es Salaam, ambaye pia mwandishi 'msaada' wa blog za habari
mbalimbali za hapa nchini na nje ya Tanzania ameanza mchakato rasmi wa
kuandika vitabu vitatu (3) vitakavyokuwa vikielezea juu ya Maisha yake.
Katika
taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Novemba 19, Andrew
Chale alibainisha juu ya kusudio hilo la kutoa Vitabu vya kuelezea
Maisha yake ni ndoto aliyonayo kwa miaka mingi na kwa sasa imetimia.
"Wengi
watajiuliza sasa nimepata wapi ujasiri wa kufanya jambo hili kubwa la
kuelezea Maisha yangu?.Ni rahisi sana, Unapokuwa na Mungu kila jambo
linawezekana hivyo vitabu hivi vitakuwa ni muongozo kwa Vijana wote hapa
Duniani kuelewa kuwa yale yote wanayopitia si ya kuyakatia tamaa, bali
kuangalia wapi wataweza kujikomboa na hata kuendana na hali iliyopo kwa
kujithamini, kujielewa, uvumilivu na kufikia malengo stahiki ya maisha"
alifafanua Andrew Chale.
Alivitaja
vitabu hivyo kuwa ni: "Who Is Andrew Chale?" Sehemu ya Kwanza), 'Who Is
Andrew Chale 2?"- 'Nimnukuu Nani?' (Sehemu ya Pili) na Kitabu cha
mwisho kitakachojulikana kama "Mimi ni Historia".
Akifafanua
vitabu hivyo vya 'Who Is Andrew Chale' cha kwanza na kile cha pili cha
'Who Is Andrew Chale 2- 'Nimnukuu Nani?', alibainisha kuwa vitaelezea
kwa kina Historia yake tokea kuzaliwa hadi alipofikia sasa huku cha Pili
cha 'Who Is Andrew Chale 2-'Nimnukuu Nani' kikielezea yale mambo yote
yaliyojificha nyuma ya pazia na ukakasi wa maisha aliyopambana nayo
kutoka kwa walimwengu na mwishowe anauliza "Nimnukuu Nani?".
Aidha,kwa
upande wa kitabu cha : "Mimi ni Historia" ameweza kuelezea ujumbe juu
ya Vijana kutokata tamaa na baadala yake wasonge mbele kwa magumu yote
waliyopitia, ikiwemo yeye.
"Mimi
ni Historia", mimi mwenyewe naogopa sana, kwanza kuanzia jina la
Kitabu, Nakumbuka nilimuuliza Mama yangu Mzazi juu ya jambo fulani la
kifamilia baina yake na Baba, lakini jibu alilonipa ndilo lililonifanya
nishike neno hili 'Mimi ni Historia'.
Kikubwa
kwenye kitabu hichi nitafafanua mambo mbalimbali ya kihistoria bila
shaka hata atakayesoma ambaye alipitia mambo kama yangu naye itakuwa ni
Historia" alimalizia Andrew Chale. Vitabu hivyo vyote vitajaa Historia
ya kweli, itakayotoa mafunzo kwa kila mmoja atakayebahatika kuvisoma Pia
vitakuwa ni kama mafunzo, mfano wa kuigwa, na kukuacha ki mdomo wazi na
hata kububujikwa machozi.
Aidha,
Andrew Chale, aliomba ushirikiano kwa wadau kujitokeza kumsapoti
ilikufanikisha juhudi za vitabu hivyo ikiwemo gharama za kuandaa Mswada,
mapitio na uchapaji. "Kwa sasa nipo katika andalio la Simulizi, na
lengo kuu nije nichapishe Mkuki na Nyota.Kwa sasa natafuta watu watakao
kuwa msaada wa awali wa kufanikisha dhumuni langu hili Ikiwemo ushahuri,
msaada wa kifedha, mchango wa kimawazo na mengineo. Tuwasiliane kupitia
0719076376 au 0767076376 au 0688076376 au chalefamily@yahoo.com" alimalizia Andrew Chale.
Andrew
Chale, ambaye kwa sasa anaishi Bagamoyo, Mkoani Pwani akifanya shughuli
zake hizo za Uandishi wa Habari, Pia ni Mwanaharakati wa Haki za Watoto
nchini, msanii wa masuala ya Vichekesho, Mtunzi wa filamu, maigizo na
mshahuri kwenye matamasha ya sanaa na Muziki, mbali hayo pia ni
Mjasiriamali katika Sanaa na Utamaduni ikiwemo kukuza Sanaa na Utamaduni
kwa Mkoa wa Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...