Photo Credits: Ye Olde Vivyl Shoppe
Baada ya pilika za wiki nzima, na mchamchaka wa maisha, sasa unakuja wakati wa kuburudika na muziki halisi wa zamani.
Katika kipindi hiki, utaweza "kuruka majoka" na "kula mangoma" kwa kusikiliza nyimbo ziliotamba miaka ya zamani, kupata historia ya wasanii na vikundi mbalimbali na pia kusikiliza mazungumzo na maDj na wasanii mbalimbali wa zamani.
Ungana na MixMaster Dj Luke Joe kwenye "one and two" na Mubelwa Bandio nyuma ya kipaza sauti kwenye kipindi kipya cha MISHUMAA YA KALE kitakachokujia kila Ijumaa kuanzia saa 11 kamili jioni mpaka saa 1 kamili usiku kwa majira ya Marekani ya Mashariki (5:00pm - 7:00pm EST)
Ungana nasi kupitia www.kwanzaproduction.com
MixMaster DJ Luke Joe. Photo Credits: IskaJojo Studios
Mubelwa Bandio


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. napendekeza hicho kitenge kiwe kitenge cha taifa, nina maana kinaweza kushonwa au kuvaliwa kwa mtindo wowote lakini kwa kitenge hicho kama vazi la taifa. nipeleke wapi maoni yangu? uncle nipelekee maoni haya, nimekuwa na hili wazo kwa muda mrefu sasa japo kuna wadau wachache nimeshawashirikisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...