Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.
Exavier Daudi (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa
lengo la kuangalia utendaji kazi wa kitengo cha mawasiliano.
Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.
Exavier Daudi akimueleza Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw.
Assah Mwambene kuhusu mikakati ya ofisi hiyo ya kuboresha mawasiliano ya
serikali kwa umma wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari katika
vitengo cha mawasiliano.
Afisa Habari wa Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Bw. Kassim Nyaki (kulia) akieleza kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene kuhusu mafanikio ya kitengo cha
mawasiliano cha ofisi hiyo katika kutoa taarifa kwa umma ambapo alisema hadi
sasa tovuti yao ina zaidi ya watu Elfu 8 wanaotembelea kwa siku.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kulia
mwenye Kaunda Suti) akiwaeleza baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii
katika kuboresha mawasiliano ya serikali kwa umma. Katikati ni Kaimu Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Francis Mwakapalila.
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Francis
Mwakapalila (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene wakati alipotembelea Ofisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kujionea utendaji kazi wa kitengo cha
mawasiliano serikalini. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
Watu wa ofisi hiyo Bw. Gerard Mwanilwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kulia)
akisisitiza kwa Maafisa Habari wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali kuhusu utoaji wa taarifa kwa umma kwa wakati. Kushoto ni
Afisa Habari wa Ofisi hiyo Bi. Evelyne Thomas.
Picha na Fatma Salum-MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...