Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama
akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani), moja kati ya mashine 4
za kurudufu CD feki zilizokamatwa katika eneo la Kimara
jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa wa Polisi, D/SSGT
Daniel Gingo. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), wino unaotumika kunakshia makasha ya CD feki wanazozitengeneza
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), baadhi ya CD feki zilizokamatwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), wino unaotumika kunakshia makasha ya CD feki wanazozitengeneza
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), baadhi ya CD feki zilizokamatwa
========= ======= ======= =======
KAMPUNI ya Udalali ya Msama
Auction Mart ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama ikishirikiana
na Jeshi la Polisi Kituo cha Urafiki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na
Michezo, imekamata kompyuta za kufyatua kazi feki za wasanii zenye thamani ya
mil18.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama, alisema
mitambo hiyo imekamatwa kwa ushirikiano mkubwa kati ya pande hizo tatu pamoja
na sapoti ya wasamaria wema. Alisema kopyuta, mashine na
kazi feki zenye thamani ya mamilioni ya fedha, zimekamatwa eneo la
Kimara-Machungwani, jijini Dar es
Salaam na mtuhumiwa huyo amefikishwa katika kituo cha
Polisi kwa ajili ya mchakato wa kiheria wa kufikishwa mahakamani.
Msama alisema akiwa mdau wa
masuala ya burudani kupitia kampuni yake ya Msama Promotions Ltd ambayo imekuwa
ikiratibu matamasha ya Muziki wa Injili, amekuwa akiguswa na kitendo wanjanja
wachache kunufaika na jasho la kazi ya wengine.Alisema wizi wa kazi za
wasanii mbalimbali umekuwa kikwazo cha mafanikio ya wahusika ambao licha ya
kuifanya kazi hiyo kwa muda mrefu, wameshindwa kupiga hatua kiuchumi kutokana
na wajanja hao kuingiza kazi feki mtaani ambazo huuzwa kwa bei ya kutupa.
Msama alisema kazi hiyo ngumu
ambayo imekuwa ikifanywa na kampuni yake kwa kushirikiana na wadau wengine,
anashukuru kwamba kadiri siku zinavyosogea wengi wamezidi kukamatwa kutokana na
ushirikiano ambao wamekuwa wakipewa.“Msama Auction Mart
tunachukua nafasi hii kulipongeza Jeshi la Polisi hasa Kituo cha Ubungo ambacho
wamekuwa msaada mkubwa kwetu katika vita hii ya kupambana na
wezi wa kazi za wasanii,”
alisema Msama.
Aliongeza, kwa ushirikiano
mkubwa wa Jeshi la Polisi na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo,
anashukuru kazi hiyo imekuwa ikisonga mbele kwa kazi feki kuzidi kukamatwa
katika maeneo mbalimbali ya nchi katika kulinda maslahi ya wasanii.Alisema tangu kuanza kwa kazi
hiyo ngumu ya kukabiliana na wizi wa kazi za wasanii, kampuni yake imekamata
vifaa mbalimbali vya kukamilisha kazi hiyo na kazi zenye jumla
ya shilingi bil.12.
Kama kweli serikali inataka kuwasaidia wasanii wangeanzisha itaratibu wa hatimiliki na kila msanii asajiliwe na basata. Radioni, tv, kuhojiwa, wawe wanalipwa kama wanavyofanya nchi zingine.
ReplyDelete