
Mtangazaji mkongwe wa radio anaesikika siku hizi kupitia radio EFM 93.7, Dennis Ssebo (pichani), hatimaye amejiunga na mtandao wa kijamii wa twitter, baada ya miaka yote kuweka msimamo wa kutojihushisha na mitandao ya kijami kwa kuwa alikua haoni faida zake.
Alipo ulizwa na Globu ya Jamii kwanini ameamua kujiunga, Ssebo alijibu, "Radio yangu ya EFM na hususani Manager wa Radio, Bwana Geoffrey Ndawula amenifungua macho juu ya faida za twitter,
"Hata hivyo najiunga na twitter tu. Sintojiunga na mitandao mingine kama facebook na instagram kwa sababu Bado sijaona faida zake", alisema Ssebo ambaye kitaaluma ni wakili pia.
Unaweza kumufollow Ssebo kupitia @ssebodennis
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...