Mwanamuziki Mkongwe kutoka bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta Khamis T. Kayumbu, maarufu kama Amigolas (pichani kulia enzi za uhai wake) amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Taarifa za awali ambazo chumba cha habari cha Globu ya Jamii imezipata kutoka kwa vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa marehemu Amigolas alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Moyo mpaka kufariki kwake.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Twanga Pepeta, msiba uko nyumbani kwa mama wa marehemu Mburahati, jirani na shule ya Msingi ya Mianzini.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho Jumatatu alasiri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. 
Amigolas atakumbukwa kwa sauti yake nzuri na utanashati awapo jukwaani. Wimbo "Aminata" alioutunga na kuuimba akishirikiana na Ally Choki, Msafiri Diof, Lwiza Mbuttu na Jessica Charles ni moja ya nyimbo bora za Twanga Pepeta wakati huo hadi sasa. Usikilize hapo chini.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi
-Amin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Taifa limepoteza nguli wa mziki

    ReplyDelete
  2. Rest In Peace My Friend Amigolas.

    P.Owino

    ReplyDelete
  3. RIP Amigolas!
    724

    ReplyDelete
  4. Inna lillah wainnailah Rajiun

    Wadau
    Ngoma Africa Band (FFU)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...